KAMATI YA BUNGE YA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII IPO MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo Mei 25, 2024 imeanza ziara ya kikazi Mkoani Mwanza huku ikitarajiwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya mkoa huo hususani iliyo kwenye Sekta ya Ustawi na Maendeleo ya jamii.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq amesema wapo Mkoani Mwanza kwa ziara ya siku moja ya kufuatilia utekelezaji wa Sera na mikakati ya utekelezaji wa miradi ya kijamii hususani wa Rock City Mall unaotekelezwa na Mfuko wa Jamii (PSSSF)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kwa mwaka 2024 Mwanza imeandaa zaidi ya Bilioni 8 kwa ajili ya kuwakopesha vikundi 529 vya Vijana, wanawake na wenye ulemavu ambavyo vimeshaandaliwa na Halmashauri na kwamba kinachosubiriwa ni utaratibu rasmi wa Serikali wa kukopesha.
"Mkoa wa Mwanza tunawatambua wafanyabiashara na tunaendelea kuwatengenezea mazingira bora ya kufanyia kazi kwa kushirikiana na wadau na taasisi zingine katika kuzipa ubora, hati miliki ili kuwapa uhakika wa soko wazalishaji" , amesema Mkuu wa Mkoa.
Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ametumia wasaa huo kutoa rai kwa Mkoa kuhakikisha wanaliangalia vema kundi la vijana linalojishughulisha na Ufugaji na Uvuvi kwani ndio uchumi wa watu wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.