• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Kamati ya Uwekezaji Yashauri Madini yote Yasafishwe Nchini kabla ya kusafirishwa nje

Posted on: March 26th, 2023


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Uwekezaji wa Mitaji ya Umma  imeishauri Wizara ya Madini kwamba migodi yote ambayo serikali inaubia isafishe dhahabu zake katika kiwanda cha kusafisha dhahabu kilichopo Jijini Mwanza (Mwanza Precious Metals Refinery( MPMR).

Pia Kamati hiyo imeshauri kuwa kiwanda hicho kutoa kipaumbele kwa kuwaajiri wazawa wenye sifa.

Ushauri huo umetolewa leo Machi 26,2023 na Makamu Mwenyeki wa Kamati hiyo Mhe. Vuma Augustine baada ya kutembelea na kukagua kiwanda hicho kilichopo kata ya Pasiansi Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza ambacho kimegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 16 ambapo hisa zake zinamilikiwa na Shirika la madini la Taifa,(STAMICO) kwa asilimia 25.

"Mradi ni mzuri sana ni wa kisasa na una tija, tumetembelea na tumethibitisha yote hayo, tunaipongeza Wizara ya Madini inafanya kazi nzuri sana kuilea STAMICO, wote tunafahamu kwamba mwaka 2017 kushuka chini Shirika hili lilikuwa linatengeneza hasara kubwa mpaka ilifikia kipindi sisi kama kamati tulitaka kuishauri serikali ilifute Shirika hilo.

"Lakini kwa sasa limeweka mikakati na limejipanga vizuri kupitia miradi yake, limekuwa ni shirika linalopata faida, wajibu wetu ni kuisimamia serikali na mashirika yake kuhakikisha inafanya uwekezaji wenye tija na hatimaye yalete gawio kwa Serikali."amesema Mhe.Augustine.

Aidha, ametoa wito kwa STAMICO kuendelea kubana matumizi na kufanya uwekezaji wenye tija ili waendelee kupata faida na kutoa gawio kwa Serikali.

Kwa Upande wake Waziri wa Madini Mheshimiwa Dkt.Doto Biteko amewataka watanzania wote wanaojihusisha na uchimbaji wa madini kusafisha madini hayo kabla ya kuyasafirisha nje ya nchi.

"Na huu ndiyo msukumo wetu mkubwa, tumejenga hivi viwanda si kwa kubahatisha bali viweze kufanya kazi, madini yote na dhahabu yanayochimbwa yasafishwe ndiyo yauzwe nje ya nchi." Amesema Mhe.Biteko.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • FAMILIA NI NGUZO IMARA KATIKA KULINDA MAKUZI YA MTOTO: DKT. BITEKO

    May 24, 2025
  • RC MTANDA AIPONGEZA BENKI YA NCBA KWA KUWAENZI WATEJA WAKE

    May 23, 2025
  • RC MTANDA AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA MA-DC UKEREWE NA MAGU.

    May 23, 2025
  • RC MTANDA AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA MA-DC UKEREWE NA MAGU.

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.