KATAMBI AWASIHI MAAFISA USTAWI WA JAMII KUSAIDIA WENYE ULEMAVU
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana, Ajira na wenye ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb) amewataka Maafisa Ustawi wa jamii na maafisa TEHAMA kutumia mafunzo waliyopatiwa katika kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini.
Amesema hayo leo Januari 23, 2025 mkoani Mwanza katika ukumbi wa Monarch Hotel wakati akizindua mafunzo ya mfumo wa kieletroniki wa taarifa na kanzidata ya watu wenye ulemavu kwa maafisa Ustawi wa jamii na maafisa TEHAMA wa mikoa na halmashauri.
“Ndugu zangu mafunzo mnayopatiwa leo yanaenda kusaidai wananchi na Serikali na kwa kufanya hivyo mnaenda kuisaidia jamii, wewe kama mtaalamu ukiwasaidia watu kutoka kwenye ulemavu wa asilimia 100 au 70 na akawa sawa hata kwa asilimia 15 wewe una mchango mkubwa hivyo hii kazi tufanye kwa moyo wa dhati tuweze kuhudumia watu wenye ulemavu” Amesema katambi.
Aidha, naibu Waziri amewaomba maafisa Ustawi wa jamii na maafisa TEHAMA wa mikoa na Halmashauri kutowatenga wala kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu na kuwahudumia kwa moyo na upendo kwa maana ulemavu hutokea pasipo kuomba wala kutegemea.
“Idadi ya watu wenye ulemavu kwa Mkoa wa Mwanza ni 10,896 kati ya hao wenye ulemavu wa viungo ni 5362 wenye ulemavu wa macho 1416 viziwi ni 1862 wenye matatizo ya afya ya akili ni 2004 na mwenye ualibino ni 609”, Amesema Mwaijega kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza.
Halikadhalika, Mwaijega ameeleza jinsi utekelezaji unavyofanyika kwa kuwawezesha watu wenye ulemavu na uhitaji katika Mkoa wa Mwanza kwa ujenzi wa madarasa na ugawaji wa vifaa muhimu kwa wahitaji.
“Zaidi ya losheni 13,611 zimegawiwa kwa albino kwa mwaka 2022 hadi 2024, ujenzi wa madarasa mawili kwa kushirikana na mdau Desk and Chair Foundation ili kuwawezesha wanafunzi kujifunzia zaidi, viti mwendo 52 kwa watu wenye ulemavu na fimbo yeupe 70 kwa wasioona”. Ameongeza Mwaijega.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.