Kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata dhahabu kinachojengwa mkoani Mwanza na mkandarasi mzawa wa kampuni ya Aqe Assogate Ltd kwa thamani ya shilingi bilioni 2.6 kutasaidia kuondoa wizi na utoroshaji wa dhahabu ambazo zilikuwa zikipelekwa nchi za nje na kuikosesha serikali mapato.
Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati akikagua ujenzi wa kiwanda hicho cha kuchakata dhahabu kinachojengwa jijini humo kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa dhahabu kwenda nje ya nchi kuchakatwa huku ujenzi huo ukisimamiwa na shirika la madini la taifa STAMICO
Alisema uchakataji huo ukifanyika nchini ajira zitaongezeka na kutoa dhahabu katika kiwango kinachokubalika kimataifa pia mradi huo unatekeleza maandiko ya sheria na msimamo wa Rais kuhusu yaliyokuwa yakifanyika kupeleka ajira nje.
“Kwa sasa tumezuia tunaanzisha viwanda katika nchi yetu na kuchakata malighafi zetu na dhahabu isiondoke katika udafi sambamba na kuzuia utoroshwaji”alisema Nyongo.
Akitoa taharifa ya ujenzi huo mkurugenzi wa shirika la madini la taifa Venance Mwisse amesema,thamani ya mradi wote mpaka kukamilika na uwekaji wa vifaa vya kuchakata dhahabu na ujenzi wa jengo hilo utaghalimu jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 133.4.
Naye Mkandarasi wa ujenzi wa kiwanda hicho Libaan Yasiri ambaye ni Mkurugenzi wa Aqe Assogates Ltd amesema, wanatarajia kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na hadi sasa umefika asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na kuanza uzalishaji mwezi Desemba.
Aliongeza kuwa mradi huo utatoa ajira ya moja kwa moja kwa watu 88 huku wa muda wakitarajiwa kuwa 200 wote wakiwa watanzania kasoro wataalamu saba wataoshiriki hatua ya za mwanzo .
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema ndani ya miezi miwili wamefanya kazi kubwa ambayo inachochea na kuhamasisha idara zingine kubadilisha staili na kufanyakazi kwa bidii aliongeza kuwa ujenzi huo inatimiza ndoto ya Rais na kukuza na kuleta mianya yenye tija kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.