MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI,TUMIENI MAFUNZO HAYA MKATOE HUDUMA BORA KWA WANANCHI:RAS BALANDYA
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana leo Aprili 28, 2024 amefungua kikao kazi kwa Maafisa Tarafa na Watendaji Kata kutoka wilaya zote za mkoa huo na kuwataka kuyazingatia mafunzo hayo ili wakatoe huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza na washiriki hao kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Balandya amebainisha bado baadhi ya maafisa hao hawatekelezi ipasavyo majukumu yao na kusababisha mlolongo wa kero za wananchi kutotatuliwa.
"Nikushukuru Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tawala za Mikoa -TAMISEMI kwa kutuletea mafunzo haya, Serikali inatambua umuhimu wa watumishi hawa miradi mingi imeanzia maeneo yao,"amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Amesema matarajio ya Serikali baada ya kutoa mafunzo hayo yanayotolewa nchi nzima ni kuona shughuli zote za Serikali ikiwemo miradi na huduma kwa wananchi zinatolewa kwa kiwango bora na kwa wakati na pia usimamizi na ufuatiliaji ukifanyika kwa umakini.
"Maafisa Tarafa nyie ni wasaidizi wa Wakuu wa Wilaya,hakikisheni mnatimiza vizuri majukumu yenu kwa kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo kwenye Tarafa,"Katibu Tawala Mkoa.
Pia amewakumbusha Watendaji kata kuwa wabunifu na kuweka mpango kazi wa Maendeleo ya kata na kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kupitia kwa Maafisa Tarafa.
"Ndugu Katibu Tawala wa Mkoa hadi sasa jumla ya Mkoa 16 imepata mafunzo haya tunayotoa kwa awamu,hii ni awamu ya tatu ikihusisha Mikoa ya Mwanza,Simiyu,Geita na Kagera na tunatarajia kukamilisha yote kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu",Ibrahimu Minja,Mkurugenzi Msaidizi,Idara ya Tawala za Mikoa,Tamisemi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanatolewa na Wakufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma na Chuo cha Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.