• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

MABORESHO YA USAFIRI WA MAJINI USIWAOGOPESHE WAWEKEZAJI-NAIBU WAZIRI

Posted on: November 18th, 2024

MABORESHO YA USAFIRI WA MAJINI USIWAOGOPESHE WAWEKEZAJI-NAIBU WAZIRI


Naibu Waziri wa Uchukukuzi Mhe. David Kihenzile leo amezindua rasmi jina na nembo mpya ya kampuni ya  Meli Tanzania, TASHICO na kusisitiza maboresho yanayofanywa na Serikali hayana nia ya ushindani bali ni kurahisisha maendeleo ya wananchi hivyo ni wajibu wote kuunganisha nguvu moja.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Novemba 18, 2024 ukumbi wa Kwatunza Hotel wilayani Ilemela Mwanza, Kihenzile amebainisha Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuiboresha  sekta yote ya usafiri ili kujenga uchumi imara kwa maslahi ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla.

"Serikali katika miaka hii mitatu imetoa jumla ya Tshs. trilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha miradi ya Meli kwenye maziwa na Mwanza ni Mkoa uliokaa kimkakati kwa kupakana na nchi za Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda hivyo mizigo mingi itapita hapa," Naibu Waziri.

Ameongeza kuwa mara reli ya kisasa SGR itakapo kamilika idadi kubwa ya mizigo ya kwenda nchi jirani itaongezeka kutokana na kuimarishwa kwa safari za majini na barabara na hivyo kuzidi kupanua fursa za uwekezaji.

Akitoa salamu za Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Katibu Tawala wa mkoa huo,Ndugu Balandya Elikana ameishukuru Serikali ya Rais Dkt.Samia kwa kuzidi kuboresha njia kuu za uchumi utakaozidi kuongeza kupata kwa Taifa na maendeleo ya wananchi.

"Hakuna Taifa lolote linaweza kupiga hatua bila ya kuboresha sekta ya uchukuzi,tunaendelea kushuhudia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali yetu kuanzia upanuzi wa uwanja wa ndege,usafiri wa Meli,barabara na reli ya kisasa.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya Meli Tanzania,Meja Jenerali mstaafu John Mbungo ameipongeza kampuni hiyo kwa huduma bora eneo lote la maziwa na kuwataka wazidi kuwa wabunifu katika usafiri huo wa majini.

Awali kampuni hiyo ilikuwa ikijulikana kwa jina la Kampuni ya huduma za Meli Mwanza MSCL na sasa inajulikana kwa jina la Kampuni ya Meli Tanzania TASHICO

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.