Mtemi Charles Kidora II wa himaya ya Kizumbi kutosha Shinyanga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Machifu kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ametoa wito kwa wananchi kushiriki uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa amani.
Chifu Kidora II ametoa wito huo leo tarehe 18 Septemba, 2025 katika Makumbusho ya Bujora-Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza wakati akizungumza na wanahabari kwa niaba ya Machifu wa kanda ya ziwa kufuatia kikao chao walichoketi kuwekeana mikakati ya kufanisha uchaguzi huo kwa amani.
Amesema, umoja huo umeamua kuhamasisha wananchi kujiandaa kuweka viongozi madarakani kwa nafasi za Rais, Wabunge na Madiwani na kwa pamoja wanatoa tamko la kumuunga mkono Chifu Hangaya ambaye ni mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, amebainisha kuwa wamejipanga kushiriki katika kampeni za Mgombea huyo za nafasi ya Urais anazotarajia kufanya kuanzia tarehe 11 hadi 12 Oktoba, 2025 na kwamba wataongozana naye katika vikao vyote vya kampeni atakavyofanya katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Naye, Mtemi Nshoma Haiwa kutoka himaya ya Kahama amesema Chifu Hangaya amefanya kazi kubwa nchini kama ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo hivyo anafaa kuungwa mkono kwa kumpigia kura ili aendelee kuwa kiongozi wa Taifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.