Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel ametoa rai kwa Chama cha Madalali wa Madini Nchini (CHAMMATA) kuthibiti wafanyabiashara wa Madini, Vito na Chuma kuacha utoroshaji wa Madini ili kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli na kuweza kuyafikia malengo ya Wizara ya makusanyo kupitia sekta hiyo.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo wa kizalendo leo Julai 13, 2022 wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Madalali wa Madini Tanzania (CHAMMATA) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa niaba ya Waziri wa Madini Mhe. Dkt Dotto Biteko.
Aidha, amewapongeza chama hicho kwa kupata usajiri na amewaahidi kuwa Seriikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kushirikiana nao ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu suala la kufanya biashara za Madini kwa kutumia leseni ya aina moja kokote nchini ili kulipatia ufumbuzi suala hilo katika kuboresha sekta hiyo .
Akiongea kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndugu Emil Kasagara amewapongeza CHAMMATA na amewaalika kushiriki Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Biashara Kanda ya Ziwa Magharibi yatakatofanyika kwenye viwanja vya Nyamhongolo kuanzia Agosti 1-8, 2022.
Mwenyekiti wa CHAMMATA Ndugu Jeremia Simon ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa kuanzisha mfumo wa Masoko rasmi ya Madini ambayo yameleta Maendeleo makubwa kutokana na kuondokana na biashara holela ya madini na wameachana na kutembea na fedha nyingi hali iliyokua inahatarisha usalama wao.
"Mfanyabiashara yeyote wa Madini atakayetorosha Madini, Chama (CHAMMATA) kitachukua hatua kali kwake ikiwa ni pamoja na kuishauri Tume ya Madini kumnyang'anya Leseni mfanyabiashara huyo na kuhakikisha hafanyi tena biashara ya Madini nchini" amefafanua Mwenyekiti.
Aidha, amefafanua kuwa malengo ya kuanzisha Chama cha Madalali wa Madini Tanzania (CHAMMATA) ni kuwa na daraja la kuwaunganisha wafanyabiashara na serikali kupitia taasisi zake kama Tume ya Madini ikiwa ni pamoja na kutetea na kusimamia haki za wafanyabiashara wa Madini, vito na Chuma.
"Madalali ni daraja la kuunganisha wachimbaji wa Madini na wauzaji wakubwa, ni watu muhimu sana nasi kama Tume ya Madini tunawathamini na kuwapenda mno hivyo tunaomba msimamie kanuni na Malengo mliyoridhia kwenye Katiba yenu ili Msaidie Utoroshaji wa Madini nchini." afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Nyaisara Mgaya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.