Kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa ambacho kimeleta mshtuko mkubwa kwa watanzania walio wengi, ofisi ya taifa ya takwimu itamkumbuka Rais Mkapa kwa mengi aliyofanya katika ofisi hiyo ikiwemo kukuza sekta mbalimbali zilizopelekea uchumi wa nchi kukua.
Mtakwimu mkuu wa serikali Dkt Albina Chuwa ameyabainisha hayo jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku kumi kwa wadadisi wa sensa ya kilimo, mifugo na uvuvi ya 2019/2020 yaliyowashirikisha washiriki kutoka mikoa mitano ya kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza,Geita,Kagera,Mara na Simiyu yenye kauli mbiu ‘takwimu bora za kilimo, mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Alisema hayati Mkapa amelitumikia taifa kwa weledi na uadilifu mkubwa na kuendelea kukuza uchumi wa nchi ambao kwa sasa unaendelea kukua kwa asilimia 7.0 hiyo ni kutokana na msimamo wake wa kusimamia sera za maendeleo endelevu kwa kutumia takwimu ambazo zilimwongoza wakati wa kutengeneza dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025 .
" Kipindi hicho ni Mkukut toa ,NBS ilipata nafasi kubwa sana ya kuzalisha takwimu za kufatilia na kutathimini nguzo tatu zilizowekwa wakati wa miaka ya 2000 Mkapa kwa juhudi kubwa aliiwezesha NBS Kufanya sensa ya watu mwaka 2002 baada ya kuahirishwa mwaka 1998 na 1999 kutokana el-mino hivyo nchi iliendelea kutumia takwimu za idadi ya watu ya mwaka 1988 na makisio yake hadi pale alipoamua kufanya sensa ya watu na makazi mwaka 2002 ambayo ilitupatia idadi ya watu wapatao 34.4 million kufanyika kwa sensa iliiletea heshima kubwa nchi kwani ilikuwa imeshawekwa katika kundi la nchi ambazo zilishindwa kufanya sensa kila baada ya miaka kumi " alieleza Chuwa
Aliongeza kuwa Mkapa aliweza kudhibiti mfumuko wa bei wa Taifa ambao mwaka 1984ulifikia asilimia 36. 3 hadi kufikia tarakimu moja katika kipindi cha utawala wake hivyo Kwa upande wa NBS Sensa hii itafanyika kisayansi kwa kutumia teknolojia ya kisiasa ambayo itapunguza gharama za kukusanya na kuchakata takwimu hizo kwa kiasi kikubwa sana.
Alisema Sensa ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 2007 hadi 2008 ilitumia takriban Bilion 10 kwa pande zote za Muungano huku Sensa ya mwaka 2019 na 2020 itatumia Tshs. 6.0 Bilioni baada ya kuchukue tahadhari za kupunguza gharama za kukusanya takwimu kwa kutumia teknolojia za kisasa na kuboresha takwimu za utawala, Tanzania imeendelea kufanya hivyo katika tafiti zinazofanyika katika pande zote za Muungano.
" Nitumie fursa hii kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano, EU na Benki ya Dunia kwa kutoa raslimali fedha na utaalam katika kufanikisha Sensa hii ila nitoe wito kuwa Takwimu hizi zinakusanywa kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu sura 351 na kila mwananchi anatakiwa atoe taarifa sahihi ili Serikali iweze kupanga mipango ya maendeleo endelevu katika Sekta ya Kilimo. Pia nitumie fursa hii kuwaasa wadadisi wapatao 322 nchi nzima wasome kwa bidii na maarifa na hususan matumizi ya vishikwambi katika kukusanya takwimu husika na wafahamu kuwa usimamizi wa karibu utafanyika na kama itabainika kwa mdadisi yoyote atakakiuka maadili ya ukusanyaji wa takwimu hizi kwa wakuu wa kaya sheria hii itachukua mkondo wake ipasavyo. Hivyo kila mmoja wetu atimize wajibu wake."alisema Chuwa.
Awali akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Juma Sweda amesema sekta ya kilimo ina umuhimu mkubwa katika mstakabali wa maisha ya binadamu kwa kuwa ndio chanzo cha chakula na malighafi zinazohitajika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii hivyo kupitia takwimu serikali imeendelea kuandaa mipango ya kuimarisha uchumi .
Aliongeza kuwa serikali inaendelea kuandaa mipango mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu inayolenga kuimarisha uchumi na kupunguza umaskini ambapo utekelezaji wa mipango hiyo itaongeza mahitaji ya takwimu bora kwa ajili ya kufatilia , kutathimini na kupima mafanikio yatakayopatika.
" Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo huenda kwa sasa ni ya kwanza hivyo napenda kutoa wito kwa wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara kuhakikisha sensa ya kilimo,Mifugo na Uvuvi inasimamiwa ipasavyo na kuendelea kutoa hamasa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kutoa taarifa za takwimu zilizo sahihi kwa wadadisi watakao pita katika kaya zao kwa ajili ya kukusanya takwimu hizo kuanzi Agosti hadi Septemba mwaka huu" alisema Sweda
Naye Emily Kasagala mwakilishi wa Katibu tawala mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba alisema anaishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kufanya ziezi hilo ambalo litasaidia kuwepo kwa takwimu ambazo ni za sasa na zenye uhakika ,baada ya mafunzo hayo wanafunzi ambao ni wadadisi waitendee haki serikali kwani uwepo wa takwimu unasaidia kuleta maendeleo katika sekta zetu katika kuweka mipangilio na utekelezaji wa mipango.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.