Maonyesho hayo ya kimataifa yanayohusisha nchi za ukanda wa Afrika mashariki yamefunguliwa katika ukumbi wa Rock city mall Mgeni rasmi akiwa Mkurugenzi mtendaji wa Tan-Trade Eng. Edwin Luta kwa niaba ya waziri wa viwanda Mhe. Innocent Bashugwa, lengo likiwa ni kuboresha maonyesho hayo ili yaweze kupata sura rasmi ya kimataifa.
Akifungua maonyesho hayo Eng.Luta amezipongeza nchi za Afrika mashariki kwa kushirikiana pamoja na kuandaa maonyesho yanayohusisha bidhaa tofauti tofauti kutoka katika nchi hizo ikiwemo vifaa vya ujenzi, nguo, pembejeo za kilimo, utalii na mawasiliano, vyombo vya jikoni, Elimu, madawa ya asili.
Kutokana na maonyesho hayo yatafanya wafanya biashara kupata fursa mbalimbali ili kuweza kukuza uchumi wetu na kuondoa tatizo la ajira katika nchi za Afrika mashariki.
"Madhumuni ya maonyesho haya ni kutoa fursa kwa wafanya biashara na makampuni yale ya ndani na nje ya afrika mashariki kutumia jiografia ya Mwanza katika kuongeza uwekezaji wa ukanda huu" Alisema Luta.
Aidha Eng. Luta amebainisha kuwa kutokana na maonyesho hayo kufanyika mara kwa mara yameweza kuwasaidia wafanya biashara wengi kujifunza ujuzi mbalimbali kutoka nchi jirani.
"Natoa wito kwa wafanya biashara na wawekezaji wazidi kuimarisha biashara na uwekezaji katika bidhaa tofauti, pia wito kwa viwanda vyote ili kuhudhuria katika maonyesho mengi ikiwemo maonyesho ya sabasaba ambayo ni ya kitaifa" Alisema Luta.
Mbali na huo wito Eng. Luta amesema kilimo chetu bado kinachechemea sana hivyo tunapaswa kusimamia matangazo ya biashara na ili tuweze kuzalisha zaidi tuwe na kilimo cha heka ili tuuze ndani na nje ya nchi yetu.
"Tanzania hatuwezi kutoka kwa kilimo cha jembe".
Naye Mwenyekiti wa Tanzania chamber of commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) mkoa wa Mwanza Dk. Elbariki Mmari amesema kutokana na mafanikio mbalimbali katika maonyesho hayo changamoto imekuwa kodi zisizo za halali kwa wafanyabiashara na stempu za wafanyabiashara kwani zinapatikana Dar es salaam tu.
"Naomba serikali iweze kuboresha huduma za stempu kwa kuweka makala katika mikoa mingine"Alisema Mmari.
Aidha Rais wa (TCCIA) taifa Mhe.Paulo Koyi amezungumza na kuwataka wafanya biashara na wawekezaji kuweka juhudi na jitihada zaidi katika biashara yao na kushiriki kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
"Wafanyabiashara wafanye kazi kwa makini na juhudi ili kesho na kesho kutwa Tanzania iwe nchi mahiri katika biashara ikiwa na sura mpya katika maendeleo yetu na hata binafsi"Alisema Koyi.
Pamoja na hayo Eng. Luta ametoa neno kwa wafanya biashara kwa kusema Tan-Trade imewaunga wanawake kuimarisha biashara iliyopo mipakani kwa kuunda taasisi mbalimbali ambapo asilimia 70 ya wanawake wanafanya biashara mipakani, na kutoa wito kwa serikali kuwawezesha kufanya biashara ambayo ni rasmi na kuwapongeza wanawake kwa hatua hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.