Wadau mbalimbali mkoani Mwanza wakabidhiwa masanduku 10 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti ugonjwa wa UKIMWI Tanzania.
Akizungumza wakati akimkabidhi masanduku hayo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kwa ajili ya kuwakabidhi wadau hao Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS),Dkt.Leonard Maboko alisema mfuko huo ulianzishwa rasmi mwaka 2015 na hayati Rais Mstaafu Benjamini Mkapa.
Alisema mfuko huo ni marekebisho ya tume ya kudhibiti ugonjwa huo nchini na ni sheria ya mwaka 2001 ambapo ilifanyiwa marekebisho 2015 na kuingizwa uwepo wa mfuko huo hivyo Jambo hilo ni la kisheria ,pia mfuko huo ulianzishwa kwa sababu fedha za wafadhili zimekuwa zikipungua miaka inavyokwenda kunakuwepo na upungufu wa fedha hizo ,hivyo serikali iliona Jambo la msingi ni kuwa na vyanzo vya ndani.
" Tumeondokewa na mwanzilishi wa TACAIDS lakini uwepo wetu Leo hapa ni kutokana na maono yake hivyo huu mfuko ni kwa ajili ya kuwahudumia watanzania pia asilimia 25 za fedha zinatumika kwa ajili ya kuzuia maambukizi mapya" alieleza Dkt.Maboko.
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella alisema anawaanini wadau hao kwani wanathibitisha wanania na dhamira ya dhati katika kupambana na vita hiyo ambapo katika maeneo yao wanasera ya kupambana na ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa mapambano hayo yanahitaji ufadhili na kutokutegemea ufadhili wa nje ama wadau wengine ni hatari kwa mapambano,pia utoaji wa elimu kutasaidia kuleta hali mpya tofauti ya mapambano sambamba na kuunga mkono maono ya Raisi Magufuli ya kuamini kwamba tunaweza kufanya mambo mengine wenyewe.
" Huwezi kuwa unapambana na vita ukategemea msaada tu wa marafiki kwani misaada hiyo inaweza kuja ikiwa imeambatanishwa na ajenda zingine na kusababisha vita yao isifanikiwe sana lakini kwenye hili zoezi mtu akiweka mia,mia mbili,au tano kwetu ina maana sana kwa sababu hatukuamka asubuhi tukiwa nayo hiyo kaja kutuwekea"alisema Mhe.Mongella.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.