Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhe Mhandisi Robert Gabriel amewakumbusha Wananchi Mkoani humo kuendelea kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vitendo na kujenga mshikamano kama walivyohimiza waasisi wa Muungano huo Mwl Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
Mhandisi Gabriel amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Sherehe hizo ambapo aliwaongoza wakazi wa Mkoa wa Mwanza kufanya usafi wa mazingira na uchangiaji wa damu.
"Waasi wetu Muungano walihimiza Watanzania kujenga mshikamano na kufanyakazi kwa bidii hivyo leo tunachokifanya ni kuuendeleza ndoto zao za kuliona Taifa la wachapakazi" amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.
Amesema zoezi la usafi waliofanya liwe endelevu kwa kila mmoja katika eneo lake kwani kwa kufanya hivyo tutajiepusha na Maradhi yanayotokana na uchafu kama Kipindi pindu na Maralia.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Gabriel amesema ni vizuri kuishi kwa upendo kwa kuwakumbuka Watanzania wenzetu wenye mahitaji maalum kama damu na mengineyo,hivyo zoezi la uchangiaji damu ni ishara ya upendo kwa vitendo.
Katika Maadhimisho hayo ya Miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mkuu huyo wa Mkoa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike pamoja na Viongozi wengine mbalimbali waliofanya usafi wa Mazingira na kushiriki pia zoezi la uchangiaji damu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza,Sekou Ture.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.