Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel ameongoza ki-Mkoa Maadhimisho ya Siku ya Familia Ulimwenguni kwa kuwakumbusha Wazazi kutambua malezi bora kwa watoto kwa faida ya vizazi vijavyo.
.
Mhe.Gabriel amesema hayo Mkoani Mwanza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Familia Duniani ambapo amesema wingi wa watoto waishio katika mazingira magumu umechangiwa na kuyumba kwa misingi ya malezi bora.
"Watoto wana haki zote ikiwemo kusikilizwa,kusomeshwa na kupendwa,sasa unamkuta mzazi hana muda na watoto matokeo yake wanaishia mitaani"
.
Naye Meneja wa Kituo cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu SOS Childrens, Dorothy Ndege amesema wamejipanga kushirikiana na Serikali kukabiliana na tatizo la watoto hao.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Dktr Thomas Rutachunzibwa amesema Asasi zisizo za Kiserikali wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri na Serikali katika kupunguza wingi wa Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa kutoa elimu na kugharamia Miradi mbalimbali
Katika Maadhimisho ya siku ya Familia Duniani Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ametoa msaada wa vyakula mbalimbali na kuahidi kushirikiana na Vituo vyote vya kulea watoto wanaoishi mazingira magumu vilivyopo Mkoani Mwanza.
Mkoa wa Mwanza una jumla ya Vituo 20 vinavyowalea watoto 602 wanaoishi katika mazingira magumu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.