MONDULI YAIMWAGIA SIFA MWANZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Halmashauri ya wilaya ya Monduli wapo Mkoani Mwanza kwa ziara ya mafunzo hususani wilayani Nyamagana katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambapo wamepikwa kwa siku 3 kwenye namna gani wanatekeleza miradi ya maendeleo kwa ufanisi.
Akiongea kwa bashasha, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa usimamizi mzuri wa miradi uliofanikisha wao kujifunza kwa kina na mna bora ya kuendeshesha halamshauri kwenye eneo hilo.
Amesema, wamejifunza mengi kwenye ziara hiyo hususani mradi wa Vizimba wa Vijana walioutembelea kwenye mwalo wa Luchelele katika kata ya Nyegezi kwani vijana hao wamewezeshwa fedha nyingi na wameendelea kusimamiwa na kupewa muongozo uliniandikia.
Ameongeza kuwa uimara wa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwenye usimamizi wameuona kwa macho kwani walikua naye katika ziara hiyo na ameonesha umahiri wa kuelezea fedha na muda halisi wa utekelezaji wa mradi jambo lililowapa funzo ya kwamba Mkurugenzi na Wakuu wa Idara wapo naye sambamba wakati wote.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Mkoa huo unatekeleza miradi lukuki kwenye ardhi na majini ikiwa ni katika kuhakikisha wananchi wanakua salama na uhakika wa miundombinu ya maendeleo.
Mhe. Mtanda ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa na Serikali kama Ujenzi wa Meli ya kisasa na Vivuko kwa ajili ya kusafirisha abiria kwenye visiwa pamoja na Soko la Kisasa, Reli ya SGR, Hospitali na upanuzi wa bandari ya Mwanza Kaskazini na Uwanja wa Ndege ambao utapandishwa hadhi kuwa wa Kimataifa.
"Sasa hivi Mkoa wetu wa Mwanza unafanya mkakati wa kuhuisha masuala ya utalii na ndio maana wenzetu wa NSSF wamejenga hoteli ya kisasa kubwa kwa ajili kuhudumia wageni wa kimataifa" Amefafanua.
Aidha, ameongeza kuwa wana Mwanza wanaongozwa na umoja na ushirikiano ndio siri ya mafanikio na maendeleo ya kasi hivyo wana Monduli na hata Arusha wanapaswa kujikita kwenye ushirikiano.
Ziara hiyo imejumuisha Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya Wakuu wa idara wa Halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.