Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amewataka Maofisa afya, waganga wakuu wa wilaya, kamati ya ulinzi na usalama,viongozi wa bandari na viwanja vya ndege kuhakikisha wanajikita katika kudhibiti ugonjwa wa ebola.
Mhe. Mongella ameyasema hayo wakati wa kikao cha kamati ya huduma ya afya ya msingi ya kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauingii nchini hasa Mwanza kwa kuwa ni Mkoa ambao ni kitovu kikubwa cha biashara hivyo kuna muingiliano mkubwa wa watu kutoka nchi nyingine.
Mhe.Mongella ameagiza kuweka vifaa tiba maalumu katika vituovya afya na maeneo yenye msongamano wa watu,pia vifaa hivyo vitawanywe ili kuweka tahadhali ya kuepuka ugonjwa wa ebola ambao ni hatari kwa sasa kwa kuwa tayari umeishaingia Nchi jirani.
" RMO vifaa tulivyo navyo visikae kwenye hospitali ya Mkoa tu bali visambazwe kwenye vituo vilivyopo maeneo hatarishi kama Nyegezi, Buzuruga,soko la Butimba na maeneo mengine yenye watu wengi hapa tupo kuchukua hatua za kujikinga" alisema Mongella.
Naye Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja alisema umakini unahitajika ili kutambua dalili zake ambazo baadhi ni homa za mara kwa mara, kutoka damu sehemu zote za mwili zilizo wazi (matundu) ikiwa upatikanaji wake waweza kuwa kwa kugusana, mate, damu, kinyesi na majimaji kutoka kwa mgonjwa, kujamiana na watu tofauti .
Akielezea changamoto zinazowakabili ni kutokuwa na kituo cha Kuhudumia wagonjwa wa milipuko ukiwemo wa ebola, ukosefu wa vifaa vya kujikinga wakati wa kutoa huduma, mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali hasa soko la mwaroni pamoja na uelewa mdogo kwa jamii juu ya ebola, pamoja na mila na desturi.
Kiteleja aliongeza kuwa mpaka sasa maeneo ambayo ni hatari ni soko la mwaroni kirumba, uwanja wa ndege wa Mwanza, bandari, vituo vya mabasi ya abiria,ukerewe na visiwa vyote, nyumba za kulala wageni, waganga wa jadi, nyumba za ibada na maombezi pamoja na vituo vya kutolea huduma za afya.
Jumhuri ya kidemkrasia ya Congo (DRC) ndio ugonjwa ulipo kwa sasa na tayari wagonjwa 34 wamepatikana na vifo 18 ikiwa ni Sawa na asilimia 52.9 baada ya kuripotiwa kuwepo kwa ugonjwa huo mei 11 mwaka huu ukiwa ni mlipuko wa tisa katika miongo minne iliyopita.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.