MWENGE WA UHURU KUANGAZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA LEO
Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mapema leo tarehe 14 Julai, 2023 imepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Ilemela tayari kwa kuukimbiza kwenye Miradi Sita yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7
Akizungumza kwenye mapokezi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Igoma, Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Amina Makilagi amebainisha kuwa wamejiandaa vema kuukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kufika kwenye miradi 6.
Mhe. Makilagi amefafanua kuwa, uwapo wilayani humo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwenye eneo la umbali wa KM 37.7 ardhini na kwamba wana ari na shauku kubwa ya kuukimbiza ili umulike na kuangaza miradi inayomeremeta.
"Mwenge wa Uhuru utapokuwa kwenye Wilaya yetu leo utaweka mawe ya msingi kwenye miradi mitatu, kufunguliwa miwili pamoja na mmoja utakaozinduliwa na miradi yote hiyo inang'ara na kupendeza." amefafanua Mhe. Makilagi.
Naye, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla Shaib Kaim ameomba ushirikiano kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na akawataka kuwa wazalendo kuipinga rushwa kwa vitendo ili kuunga juhudi za Mhe. Rais za kuleta maendeleo nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.