OFISI YA MKUU WA MKOA ITAHAKIKISHA HAKI ZOTE ZA WATU WENYE ULEMAVU ZINALINDWA NA KUTEKELEZWA-RC MAKALLA
*Awaahidi kutengewa maeneo ya biashara maeneo ya Masoko*
*Ashauri Mwanza kwenda kujifunza soko la Machinga Complex kuhusu kuwatengea vizimba watu wenye ulemavu*
*Usalama wao ndiyo kipaumbele cha kwanza*
*Ampongenza Mbunge wa viti Maalum Mhe. Khadija Shaaban kwa uwajibikaji mzuri kwa makundi maalum*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.CPA Amos Makalla amewakikishia watu wenye ulemavu Mkoani humo kuzilinda na kuzitekeleza haki zao zote wanazostahili kama watu wengine likiwemo kutengewa maeneo yao ya biashara kwenye Masoko na usalama wao kwa ujumla.
Amesema hayo leo wakati wa mazungumzo ya pamoja na wawakilishi wa Vyama vya watu wenye ulemavu na kula nao pamoja chakula kwenye ukumbi wa Mwanza Hotel ambapo amesisitiza hakuna nafasi ya mtu yoyote kubaguliwa kutokana na kasoro yake ya kimaumbile na wachache wanaofanya hivyo watambue mkondo wa sheria utawapitia.
"Nimekaa hapa nimewasikiliza wote mnaowawakilisha wenzenu changamoto zote mnazopitia,narudia kusema nimeyapokea na nitakwenda kuyafanyia kazi kasoro tu yale ya kisera na sheria,"CPA Makalla.
Amesema alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Da r-e.s-Salaam ametengeneza mazingira mazuri kwenye soko la Machinga Complex kwa kuwatengea maeneo rasmi watu wenye ulemavu, hivyo na kutaka Mkoa wa Mwanza ujifunze kwa mpango huo.
Mhe. Makalla amesema amesikia kilio cha Vyama hivyo kukosa Ofisi za kufanyika kazi hivyo suala hilo ameagiza litekelezwe haraka kwenye majengo yote ya Taasisi za Serikali wapatiwe nafasi.
"Tayari Rais wetu Dkt.Samia Suluhu ameshatoa maagizo hayo hivyo hakuna sababu ya kusua sua au kujadiliana wahusika wote mhakikishe viongozi hawa wa vyama vya walemavu wanapatiwa Ofisi za kufanyia shughuli zao,"amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha amewatahadharisha wale wote wanaotoa lugha zisizo na staha kwa watu wenye ulemavu wakiwemo Albino kuwacha tabia hiyo na wanaowakataa kuingia kwenye vyombo vya usafiri LATRA na RTO wawachukulie hatua za kisheria
"Mhe.Mkuu wa Mkoa huu ni utaratibu niliojiwekea wa kuzunguka mikoani na kukutana na makundi maalum ninayoyawakilisha Bungeni,kusikiliza changamoto zao na kwenda kuzisemea ili ufumbuzi upatikane,"Khadija Shaaban maarufu kama Keisha,Mbunge wa viti maalum.
"Sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupigania usawa wa wananchi wote,na kwa kupitia Mkutano huuu tunazidi kupata mengi ya kujifunza na kuyatekeleza," Mhe.Stanslaus Mabula,Mbunge wa Nyamagana.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.