PAMBA JIJI FC YAPATA MAPOKEZI YA AINA YAKE, JIJI LAZIZIMA KWA SHANGWE BAADA YA KUFUZU LIGI KUU MSIMU UJAO
Furaha, vifijo, nderemo na kila aina ya shamrashamra vimetawala wakati wa mapokezi wa timu ya soka ya Pamba Jiji FC wakati ikiwasili ikitokea Arusha baada ya kufuzu kucheza ligi kuu msimu ujao.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda aliipokea timu hiyo eneo la Misungwi na kuambatana na timu hiyo maeneo mbalimbali kabla ya kuingia eneo rasmi la tukio.
Funga kazi na shughuli mbalimbali kulazimika kusimamia kwa muda ilikuwa mara baada ya timu hiyo kuingia viunga vya Jiji la Mwanza na kuanza kukatiza kwenye barabara za Pamba, Buzuruga Nyasaka, Makongoro hadi kuingia uwanja mkongwe wa Nyamagana.
Mhe. Said Mtanda aliyeonekana kuzidiwa kwa furaha amebainisha kuwa sasa ni wakati wa kuiweka timu ya Pamba Jiji katika hadhi ya ligi kuu huku akitangaza rasmi dimba la Nyamagana kuwa la nyumbani kwa timu hiyo.
"Mkurugenzi wa Jiji awali ya yote nakupongeza sana nimeona juhudi zako sasa nataka kuona majukwaa kwenye uwanja huu na taa ili mechi za usiku zirindime humu," amehimiza mkuu huyo wa Mkoa mkereketwa wa soka.
Amesema ligi kuu ina hadhi yake, Pamba Jiji Ina historia nzuri katika ramani ya soka, ni lazima iwe na majengo yake ya klabu na hosteli za kisasa.
"Mechi zote kasoro za Simba na Yanga zitapigwa hapa Nyamagana,huu ni miongoni mwa viwanja bora unahitaji marekebisho kidogo na tutaishuhudia timu yetu ikisukuma gozi la ng'ombe humu huku timu zikitoka na vichapo," amesema Mtanda huku akishangiliwa na umati wa mashabiki waliofu rika uwanja I hapo.
Mkuu huyo wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza unaomiliki timu hiyo kuhakikisha unaunda safu imara ya watu wa kuliongoza timu hiyo hhuku wachezaji wa zamani nao wakipewa nafasi za heshima za kuingia uwanjani na ushauri kwa Pamba Jiji.
"Hongera sana Mkuu wetu wa Mkoa umetuheshimisha sana,pia hongera zake mtangulizi wako comrade Amos Makalla wote kwa pamoja mmefanya kazi kubwa",Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Awali, timu hiyo maarufu kama TP Lindanda mara baada ya kupokelewa Wilayani Kwimba eneo la Hungumalwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Ng'wizalubi Lidigija.
"Hutushuki tena,..Pamba oyeeee sasa tumepata burudani tuliyoikosa miaka mingi karibuni majembe wetu kazi tumeiona asanteni," ni kauli za mashabiki wa soka walipopaza sauti kwa wachezaji wa Pamba Jiji FC.
Pamba Jiji FC ilianzishwa rasmi mwaka 1984 na kufuzu ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka 1984 kabla ya kushuka daraja mwaka 2000.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.