Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watumiwa sugu 46 wanaojihusisha na makosa mbalimbali yakiwamo unyanganyi, kupatikana na dola bandia ,wizi wa vifaa vya magari,utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alisema kati ya watuhumiwa hao wamo wahalifu sugu 21 wa matukio ya unyaganyi wa injivi za wavuvi ndani ya Ziwa Viktoria katika maeneo ya kisiwa cha Kunee, Bwiro, Kweru na Ilugwa, Bezi na Makoba vilivyopo wilaya ya Ukerewe na Ilemela.
Alitaja maeneo yalivamiwa na wahalifu hao ni visiwa vya Kasarazi, Zilagura, Iyozu na Maisome wilayani Sengerema ambapo watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na injini 21 za mitumbwi, nyavu haramu 195 na pikipik mbili.
“Katika msako huo kwa nyakati tofauti tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wa makosa ya utapeli wa dolla bandia za Marekani noti 599 ambapo kila moja ni dola 100.
“Vile vile tuliwakuta na noti 32 za Sh 10,000 za Tanzania ambazo ni sawa na Sh 320, 000 kama zingekuwa halali, watano kati ya hao walikamatwa wilayani Nyamagana na mmoja aliyekuwa na dola alikamatwa Sengerema.
“Pia tumewakama wezi tisa wa vifaa vya magari yaani vipuri kwenye makazi ya watu, walikutwa na ushahidi mbalimbali ikiwemo taa za magari, vitasa, radio za gari na vioo,” alisema Muliro.
Aliwataja baadhi ya watu wanaoshikiliwa na kusubiria upelelezi ili kufikishwa mahakamani ni Muhoja Magendo, Peter Timoteo, Dotto Malemu, Mashaka Masanja, Emmanuel Zafania, Joseph Daniel, Fred Daniel, Oscar Haji, Samwel Paulo, Rajab Ibrahim, Tomas Christopher.
Wengine ni Phinias Elija, Shaban Nassoro, William Yamo, Issa Ngoreke, Elias john, Mariam Joseph, Yusuph Lukanyaka na Chausiku Wankuru.
Hata hivyo Kamanda Murilo alionya baadhi ya watu kutojihusisha na vitendo vya uhalifu na kuwataka kufanya shughuli zao halali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.