*PS3+, TAMISEMI WAZIJENGEA UWEZO SEKRETARIETI ZA MIKOA KANDA YA ZIWA NA KASKAZINI*
Mradi wa miaka mitano wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma Awamu ya Pili (PS3+), unaofadhili na Serikali ya Marekani na kutekelezwa kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la watu wa Marekani (USAID) na kuwezeshwa na Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) kwa Kushirikiana na OR- TAMISEMI wawajengea uwezo Maafisa kutoka Sekretarieti za Mikoa Jijini Mwanza.
Akizungumza leo Disemba 04, 2023 Jijini Mwanza kwa niaba ya Shirika la PS3 Mkurugenzi wa Ufuatiliaji, tathmini na ujifunzaji wa Shirika hilo Ndugu Sono Kusekwa amesema wameamua kutaasisisha mambo yote yanayofanywa na Shirika hilo nchini ili wawe na weledi na kupata muendelezo wa kilichokusudiwa kwa kipindi chote cha mradi na hata baada ya kuondoka kwa shirika hilo.
Serikali ya Marekani kupitia PS3+ ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini kwani amekua na dahari ya miaka akishirikiana na Serikali katika kuimarisha mifumo ya utendaji kazi kama PLANREP, LGRCIS, EPICOR, FFARS, GWF na GOTHOMIS. Kikao kazi hicho kwa Maafisa TEHAMA, Mipango, Wakaguzi na Ufuatiliaji kutoka Sekretarieti za Mikoa kanda ya Ziwa na Kaskazini kitadumu kwa siku tano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.