RAIS SAMIA ATOA ZAIDI YA BILIONI 30 KUJENGA VIVUKO VIPYA MWANZA: RC MAKALLA
*Amshukuru Mhe. Rais kwa kuboresha usafiri wa majini*
*Awataka TEMESA kumsimamia mkandarasi kukamilisha ujenzi*
*Awapongeza Songoro Marine kwa uhodari na kujenga boti za uokozi Ukerewe*
*Amezitaka Halmashauri kutatua changamoto za vituo vya ufuatiliaji*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla leo Januari 10, 2024 amekagua ujenzi wa vivuko vipya vitano vinavyojengwa kwenye karakana ya Songoro Marine Wilayani Ilemela kwa zaidi ya Bilioni 30.
Akiongea na uongozi wa mkandarasi huyo pamoja na wasimamizi (TEMESA) Makalla ametumia wasaa huo kumpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha hizo kujenga vivuko vipya vitakavyoimarisha usafirishaji ziwani.
Amesema, awali wananchi waishio kwenye visiwa walipata shida kusafiri kwa kutumia mitumbwi jambo lililohatarisha usalama wao lakini kukamilika kwa vivuko hivyo kwa pamoja mwishoni mwa mwezi Machi 2024 kutaimarisha usafiri.
"Wananchi wetu siku za nyuma walitumia vivuko visivyo na uhakika, uwekezaji huu mkubwa wa Mhe. Rais wa zaidi ya Bilioni 30 kujenga vivuko hivi vipya utasaidia kuimarisha usafiri kwenye visiwa hususani Ukerewe, Magu na Sengerema." Mkuu wa Mkoa.
Aidha, amempongeza na kumshukuru mkandarasi Songoro Marine Co. Ltd kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa uaminifu na akawataka TEMESA kulipa fedha kwa wakati na kusimamia usiku na mchana ili kazi ikamailike kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
Awali, Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine Major Songoro ameahidi kujenga kwa kasi na kukamilisha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba ili wananchi wanaovisubiri wapate uhakika wa usafiri kwenye maeneo na kwamba vyote kwa pamoja vitakamilika kabla ya mwezi Mei 2024.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa tunaendelea na ujenzi wa vivuko vya Rugezi - Kisorya kwa zaidi ya Milioni 892, Ijinga -Kihangara kwa Bilioni 5, Bwiru -Bukondo kwa Milioni 677, Nyakalilo-Kome kwa zaidi ya Bilioni 8.5 pamoja na Buyagu-Mbariika kwa zaidi ya Bilioni 3.5 na tutakamilisha kwa mujibu wa mkataba." Mkuu wa Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.