RAS Balandya aupokea Mradi wa kujitolea kutoka JICA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana leo Novemba 20, 2023 ameupokea rasmi mradi wa kujitolea kutoka Shirika la Maendeleo la watu wa Japan (JICA) ambapo wataalamu wa fani mbalimbali watakuja Mkoani humo kwa lengo la kufundisha kuanzia shule za Sekondari hadi Vyuo.
Akizungumza na viongozi kutoka JICA kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa pamoja na Wakurugenzi, Wakuu wa Idara za Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri za Nyamagana na Ilemela, Mtendaji huyo wa Mkoa amesema mradi huo ni muhimu katika harakati za kujiletea maendeleo kutokana na Taifa kuwa na wataalamu siku za usoni.
"Siri ya Taifa lolote kusonga mbele kiuchumi kwanza ni lazima liwekeze katika elimu ili kuwapata wataalamu mbalimbali watakao kuwa chachu ya kuinua uchumi",amesisitiza Balandya wakati akizungumza na wageni wa JiCA.
"Japan na Tanzania tuna miaka mingi ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu,afya na miradi ya kiuchumi, kipindi cha Uviko 19 tulisimama lakini sasa tunaendelea", Nakagawa Haki, Mratibu wa mradi JICA.
Kwa upande wake Afisa mipango wa mradi huo Bi. Mbonisewa Mtambalike amebainisha wamefika Mwanza kuzungumza na wakuu wa maeneo husika kuanzia ngazi ya Halmashauri ili kutambua mahitaji yao kabla ya utaratibu mwingine kufuata ikiwemo kuomba kibali rasmi Tamisemi.
JICA ni Shirika la Maendeleo ya watu wa Japan ambao wamekuwa na ushirikiano na Tanzania kwa miaka 60.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.