Katibu Tawala Mkoa wa Geita bw. Mohamed Gombati amewaalika wananchi kutembelea katika maonesho ya nane nane ili wajifunze mbinu bora na za kisasa katika ufugaji, kilimo, biashara na uvuvi kutoka kwa wataalam.
Ametoa wito huo leo tarehe 07 Agosti, 2025 alipotembelea katika viwanja vya maonesho ya nane nane Nyamhongolo wilayani Ilemela yanayohusisha mikoa ya kanda ya ziwa magharibi.
Ndugu Gombati amesema wakulima wakifika katika maonesho hayo watajifunza mbinu mbalimbali ikiwemo namna bora ya kulima kilimo lishe katika eneo eno dogo ambalo huzalisha mazao ya kutosha.
Aidha, amebainisha kuwa maonesho hayo mwaka huu yamekua na tija sana kwa jamii kwani kila sekta imeleta mashamba darasa hususani ya kilimo cha mazao ya muda mfupi, unenepeshaji wa mifugo pamoja na uvuvi kwa kutumia vizimba.
Vilevile, amebainisha kuwa wananchi watakaofika kwenye maonesho hayo ya saba watapata fursa ya kukutana na taasisi za kifedha na kuelikishwa juu ya furaa za mikopo midogo na mikubwa kwa makundi hayo ya wajasiriamali ambayo inalenga kuinua uzalishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.