RAS MWANZA AWAPONGEZA BODI YA MIKOPO KUJALI WENYE KIPATO DUNI ELIMU YA JUU
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewapongeza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa kuwatambua wanafunzi waishio katika mazingira magumu na Walemavu na kusaidia kutimiza malengo ya kupata Elimu.
Amebainisha leo Jumanne Machi 26, 2024 wakati wa kikao kifupi cha utambulisho wa bodi hiyo kilichofanyika kwenye Ofisi ya Katibu Tawala huyo.
"Tunafaham umuhimu wa mikopo, hususani katika familia masikini na walemavu ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za ada ya chuo, tunawashukuru kwa utaaratibu wenu wa kutambua watoto waishio katika mazingira magumu kwa kushirikiana na TASAF." Amesema Balandya.
Aidha, Balandya ameiahidi Bodi hiyo ushirikiano wa dhati kutoka kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wote watakapohitaji.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu Dkt. Bill Kiwia amebainisha kuwa zaidi ya Tshs. Bilioni 700 za mikopo kwa wanufaika bado haijakusanywa hivyo kupelekea kurudisha nyuma utoaji wa huduma hiyo.
"Kuna zaidi ya bilioni 700 bado hazijakusanywa kutoka kwa wanufaika waliopita kutokana na kuwa katika sekta zisizo rasmi, jambo hili linaturudisha nyuma kwani fedha ambazo wangekopeshwa wengine zinakosekana."Ameweka wazi Dkt. Kiwia
Halikadhalika, ameongeza kwa kuuomba uongozi wa Mkoa wa Mwanza kushirikiana nao ili kuwapata wadaiwa wote na kuweza kurudisha fedha hizo, huku akieleza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kila mwanafunzi wa chuo anakuwa mnufaika wa mikopo katika ngazi ya Elimu ya juu kwa miaka ijayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.