Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amewataka Maafisa Ushirika kutoka Halmashauri 5 za Mkoa huo aliowakabidhi Pikipiki zikatumike kama zilivyokusudiwa na kuleta matokeo chanya.
Akizungumza kwa niaba yake katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika leo nje ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Joachim Otaru amesema Serikali kwa kutambua changamoto za utendaji kazi likiwemo suala la usafiri imewapatia usafiri huo hivyo jukumu lao ni kwenda kufanya kazi kwa Weledi.
"Serikali ya Awamu ya Sita ni sikivu imesikiliza changamoto zenu na kuzitatua kwa kuwapatia Pikipiki hizi sitarajii kuona mkizigeuza kama miradi ya kuwapatia vipato tofauti na hapo hatua za kinidhamu zitawahusu" Otaru
Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoani Mwanza Lucas Kiondele amesema Maafisa Ushirika kwa muda mrefu wameshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yao ya kutoa elimu kutokana na umbali wa sehemu wanazotakiwa kwenda kufanya kazi, hivyo usafiri huo utaleta ufanisi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara amesema hizo ni hatua zinazofanywa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuwaletea Maendeleo Wananchi, ametoa Pikipiki pia kwa Maafisa Kilimo na Uvuvi.
Pikipiki hizo zimetolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa Maafisa Ushirika kutoka Halmashauri za Magu, Misungwi, Kwimba, Sengerema na Ukerewe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.