RAS MWANZA AWATAKA WATENDAJI KUTUMIA MIFUMO KUBORESHA HUDUMA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka watendaji kwenye mamlaka za Serikali za mitaa kutumia fursa ya uwepo wa mifumo kuboresha huduma zao katika kuhudumia wananchi.
Ametoa wito huo leo wakati wa kikao kazi cha Maafisa TEHAMA, usimamizi wa fedha, mipango na usimamizi na ukaguzi kutoka Mikoa 10 ya kanda ya Ziwa, kaskazini na kati kinachoratibiwa na TAMISEMI chini ya ufadhili wa mradi wa USAID PS3+.
Balandya amesema huko nyuma TAMISEMI ilisimamia mifumo yote lakini sasa wataalamu wapo kwenye kila mamlaka inayotumia hivyo ni fursa kwa wataalam hao kuitumia katika kuboresha huduma wanazotoa kwa jamii.
"Yatumieni mafunzo haya ya siku tano vizuri kwani ni wajibu wetu kusimamia mifumo kutekeleza shughuli za wananchi kwa ufanisi kwa kuboresha huduma tunazotoa" Amesema Balandya.
"Hii ni mara ya pili tunawawezesha maafisa wa sekretarieti za mikoa ili waweze kusimamia utekelezaji wa mipango na bajeti ili nao wakasimamie vizuri Halmashauri kwa kutumia mifumo" Amesema Ndugu Johnson Nyingi kutoka TAMISEMI.
Naye, ndugu Sono Kusekwa kutoka USAID PS3+ mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani na kutekelezwa kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la watu wa Marekani (USAID) unaowezeshwa na Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI (PEPFAR) amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha mifumo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.