Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Adam Malima amewakumbusha wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kusimamia vyema majukukumu yao kutokana na kamati hiyo kuhusika na masuala muhimu ya Maendeleo kwa mwananchi.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo leo kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Mhe Malima amebainisha Kamati hiyo imebeba majukumu ya Wizara kadhaa ikiwemo Afya na Elimu eneo ambalo ndiyo msingi wa maendeleo na kuwataka kutofumbia macho yale yote watakayobaini hayana tija kwa mustakbar wa Taifa letu.
"Mmekuja Mwanza mkianzia kuikagua Taasisi ya TMDA ambayo ipo chini ya Wizara ya Afya,hii ni Taasisi inayojihusisha na dawa na Vifaa Tiba mkazifanyie kazi changamoto zote mtakazoziona ili kuendelea kumpa usalama mwananchi" amesema Mkuu wa Mkoa.
Amewaambia wajumbe hao wa Kamati ya Bunge kuwa miongoni mwa kitega Uchumi cha Mkoa wa Mwanza ni Uchumi wa Bluu,zipo hujuma za hapa na pale za kukwamisha Uchumi huo hayo yote ni ya kuyafanyia kazi, mkajiridhishe na kuyapatia ufumbuzi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Aloyce Kamamba amesema wanatambua uzito majukumu yao,wamekuja Mwanza kukagua na kujiridhisha na kazi zinazofanywa na TMDA ili baadaye waje kulishauri Bunge pale watakapoona kuna haja ya kuchukua uamuzi huo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii inasimamia Sekta ya Afya,Elimu,Wanawake,jinsia na Makundi Maalum,Maendeleo ya Jamii pamoja na Michezo na Sanaa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.