RC MTANDA AIPONGEZA BENKI YA NCBA KWA KUWAENZI WATEJA WAKE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ametoa pongezi kwa Uongozi wa Benki ya NCBA kwa kuandaa jioni maalumu kwa ajili ya kuwaenzi wateja wake wa thamani huku akisema hatua hiyo inakumbusha taasisi za kifedha na zingine kuwa kuna haja ya kuwapa heshima wateja wake.
Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo usiku wa leo Mei 23, 2025 alipokuwa akizungumza katika tukio la chakula cha jioni kwa ajili ya wateja wa Benki ya NCBA lililofanyika katika ukumbi wa Gold Crest Hotel ambapo ameipongeza benki hiyo kwa kuja na wazo la kuchangamana na wateja wake.
“Uwepo wa wateja hapa leo ni moyo wa maendeleo ya benki ya NCBA, pia ni moyo wa kanda ya ziwa,.biashara zenu, Uwekezaji wenu, mawazo yenu, ndoto zenu, vyote vinachangia ukuaji wa uchuki wa Mkoa wa Mwanza na Taifa kiujumla." Amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, ameipongeza benki hiyo kwa kuja na jukwaa jipya ka huduma za kibenki mtandaoni na kampeni ya mpya ya Maisha ni Hesabu, hii ikiwa ni dalilo ya wazi kuwa benki iliyo ya kisasa inayojali na inayoangalia mbele.
Tutaendelea kuhakikisha mnaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wetu. Tutahakikisha mazingira yanaendelea kuwa salama na rafiki kwa biashara na uwekezaji wenu.
Amesema Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hayo Mhe. Mtanda amesema juhudi kubwa zimefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha Sekta ya fedha na hususani Maendeleo ya Kibenki. Hivyo, wao katika Serikali ya Mkoa wataendelea pia kuweka mazingira mazuri ya kila mfanyabiashara kutekeleza majukumu yake bila kuvunja sheria.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.