Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 18 Novemba 2025 ameupokea ugeni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Unaoshughulikia Maafa waliofika Mkoani humo kuangalia utayari wa kuanzishwa kwa kamati za maafa.

Alizungumza na ugeni huo Mhe. Mtanda amewapongeza kwa kazi nzuri ya kujali jamii huku akibainisha kuwa kuweka mikakati na mipango ya kukabiliana na maafa ni kujali jamii moja kwa moja tofauti na kusubiri maafa yatokee.

Aidha, ametumia wasaa huo kuwataka wataalamu wanaounda timu ya Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Mkoa huo kuhakikisha wanafanya kazi hiyo nyeti kwa ufanisi kwani maafa hayabishi hodi hivyo ni lazima wawe tayari kusaidia halmashauri na jamii hususani kutoa elimu wakati wote.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Itafiti Idara ya Menejimenti ya Maafa Ndugu Vonyvavo Luvanda ambaye ameiongoza timu hiyo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu amesema ziara yao mikoani inalenga kuangalia maandalizi ya awali kama uwepo wa timu za maafa na chumba maalumu ili kukidhi matakwa ya wahisani wanaoshirikiana na ofisi hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inalenga kuwa na timu za maafa katika ngazi za Halmashauri na Mikoa yote nchini na kwamba wahisani wa zoezi hilo ni Benki ya Dunia (WB) pamoja na mashirika mengine na kwamba kwa Mwanza UNDP ndio wafadhili wakuu.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.