RC MTANDA AISHUKURU BAKWATA KUANDAA DUA KWA AJILI YA RAIS SAMIA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amelishukuru Baraza la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) kwa kuandaa Dua maalum nchi nzima kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza Taifa kwa hekima na kumuepusha na mabaya.
Dua hiyo iliyofanyika leo Januari 31, 2025 kwenye viwanja vya Bakwata eneo la Mbugani wilayani Nyamagana Mtanda amesema viongozi wetu wanahitaji kutiwa moyo kwani kazi ya kuliongoza Taifa ni kubwa hivyo inahitaji maombi kama hayo.
"Nitoe shukran za pekee kwa Mufti Zuberi bin Ali Mbwana kwa kutoa maelekezo haya ambayo leo tunayashuhudia yakitekelezwa mkoani kwetu,siku zote Dua ni chakula ya moyo pia ni ulinzi kwa lolote baya," amesisitiza mkuu huyo wa mkoa.
Mtanda amesema Rais wetu anaendelea kufanya mengi mazuri ya kujenga uchumi wa Taifa letu lakini pia wapo wachache wasiofurahishwa hivyo njia sahihi ni kuendelea kumuombea fua mara kwa mara hali ambayo itazidi kumuongezea ari ya kulitumikia Taifa kwa weledi.
"Tunaona mengi anayofanya Rais wetu,hapa Mwanza ametuletea miradi mingi ya maendeleo kuanzia sekta ya afya,elimu na miundombinu,tuna kila sababu ya kumuombea kiongozi wetu,"Hassan Kabeke,"Sheikh wa Mkoa wa Mwanza.
Dua hiyo iliyowajumuisha pia viongozi wa madhehebu mengine imeongozwa na Sheikh Abuu Ladhwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.