RC MTANDA AKOSHWA NA BONANZA LA USHIRIKA NA Mabeki
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amepongeza ubunifu wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza kwa kuja na jukwaa la michezo lililowakutanisha Vyama vya Ushirika pamoja na Mabenki lililolenga kuimarisha ushirikiano.
Akitoa salamu za ufunguzi wa Bonanza hilo leo Mei 14, 2025 katika viwanja vya mpira wa miguu Nyamagana, Mhe. Mtanda amesema anawapongeza Ushirika Nyanza kwa kuona umuhimu wa kuchangamana hususani na Taasisi za Kifedha kwa kuwa ndio washirika wao wakuu na wanafanya kazi kwa karibu.
“Mnapokua katika ushirika mnazungumzia kuhusu masula ya uchumi na maendeleo lakini muwapo hapa mnaimarisha afya na mahusiano”. Mhe. Mtanda.
Sambamba na hayo, RC Mtanda ametoa wito kwa wanaushirika kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha Vyama vya Ushirikiana na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuunga mkono juhudi na jitihada za kujenga Ushirika Mkoani Mwanza.
Mbali na hayo Mhe. Mtanda amewaomba Wanaushirika kuiunga mkono benki ya Ushirika Tanzania ambayo ilizinduliwa Aprili 28, 2025 na Mhe. Rais Dkt. Samia na kuwataka Wanaushirika na wasio wanaushirika kutembelea benki hiyo na kupata huduma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.