RC MTANDA ASHUKURU MCHANGO WA SEKTA BINAFSI KWA JAMII, APONGEZA ULIPAJI KODI
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Comrade Christopher Ngubiagai ameahidi kuendeleza ushirikiano na sekta binafsi yakiwemo mazingira rafiki ya shughuli zao ili wawe walipa kodi bora na kuongeza pato la Taifa.
Akizungumza wakati wa utoaji wa misaada kwa jamii kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 11 ya kampuni ya Usafirishaji ya Gaini Ltd Ngubiagai amesema Mwanza inajivunia mchango wao kukuza uchumi.
"Nawapongeza Gaini Co. Ltd kwa kuwa walipa kodi wazuri tena kwa asilimia 100 na sehemu ya faida yenu kuirudisha kwa jamii huu ni mfano wa kuigwa,na hii imechangiwa na Serikali ya awamu ya 6 ya kuwawekea mazingira mazuri sekta zote binafsi hapa nchini", Mkuu wa Wilaya.
Ameendelea kusema kuwa Mkoa wa Mwanza ambao unazidi kuimarika kwa vitega uchumi, wafanyabiashara watakuwa na fursa nzuri ya kuwekeza na kutanua wigo wa kazi zao na Mataifa ya jirani na nje ya nchi.
Ngubiagai katika sherehe hizo ameshiriki zoezi la utoaji wa mahitaji maalum kwenye kambi ya kulea wazee huko Misungwi, msaada wa mashine ya Photokopi, Viti 32 na meza kwenye shule ya Sekondari ya Nyakabungo na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 2 wilayani Ukerewe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Gaini Peter Chacha amesema vitu vyote hivyo vina thamani ya zaidi ya Tshs. milioni 15 na wametoa kwa jamii katika sehemu ya faida wanazopata lengo likiwa ni kujenga upendo na ushirikiano na wananchi na kuondoa hali ya unyonge kwa wale wasiyo jiweza.
"Ndugu mgeni rasmi huu ni utaratibu tuliyo jiwekea wa kujenga ukaribu na jamii inayotuzunguka tukiamini mshikamano ndiyo silaha ya kusonga mbele na kupata mafanikio", Mkurugenzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.