“Mara nyingi mnavyopewa vifaa kama hivi mnavichukulia kama vifaa vyevu na sio vya umma hivyo ninawataka muende mkavitunze, nishati ya umeme wa jua mkatumie kwenye vituo vya afya na zahanati na sio kubandika majumbani kwenu”.
Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda aliyoitoa leo Julai 25, 2025 wakati wa hafla fupi ta kukabidhi baiskeli 433 na mifumo ya umeme wa jua kwa ajili ya Vituo vya afya Mkoani Mwanza, huku akiwataka wanufaika kuvitumia kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa na kutunzwa vizuri ili viendelee kutumika kuongeza ufanisi na utoaji huduma za afya.
Mhe. Mtanda amesema Baisikeli hizo zenye thamani ya Shilingi milioni 112,355,706 zinalenga kusaidia kuboresha utoaji huduma ikiwemo, ufuatiliaji na huduma kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kutokana na umbali mrefu na wengine kushindwa kufika katika vituo vya afya.
“Baiskeli hizi zitatumika na wafanyakazi wa huduma za afya kufuatilia wateja ambao hawajahudhuria katika kituo cha afya, kusambaza dawa za ARV kwa wateja, kufanya upimaji wa virusi vya UKIMWI”.
Mifumo hii ya umeme wa jua yenye thamani ya Shilingi bilioni 1,559,715,171.65 itafikia zaidi ya vituo 110 katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni kuhakikisha nishati endelevu katika utoaji wa huduma za afya. Amesema Mkuu wa Mkoa.
Basikeli na vifaa vya umeme wa jua vilivyotolewa kwa ajili ya vituo vyetu vya afya mkoani Mwanza vimetolea shirika la ICAP kwa ufadhili wa CDC na PEPFAR vitakavyosaidia utekelezaji wa afua za UKIMWI mkoani Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.