RC MTANDA AWASHUKURU WANANCHI SENGEREMA KWA MAPOKEZI MAZURI YA KATIBU MKUU WA CCM
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Sengerema kwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyewasili Mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Mhe. Mtanda ametoa shukrani hizo wakati alipokuwa akitoa salamu za Serikali ya Mkoa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani Wilayani Sengerema, RC Mtanda amesema ni heshima kubwa kwa wananchi hao ambao wamejitokeza ikiwa ni kuashiria kushukuru kwa yale mengi mazuri yaliyofanywa na Chama hicho.
Aidha, Mhe. Mtanda amemuhakikishia Katibu Mkuu huyo usalama wa hali ya juu kwa kipindi chote atakachokuwepo katika Mkoa huo yeye pamoja na msafara wake, na kumtoa hofu kuhusu hali ya vurugu kwani jeshi la polisi Mkoani humo limejipanga kuhakikisha usalama unaimarishwa kwa kipindi chote
"Nimesimama hapa pia kukuhakikishia Katibu Mkuu kwamba hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Mwanza ni shwari kabisa kabisa, wewe na msafara wako mtafanya kazi yenu ya kisiasa katika Mkoa huu bila tishio lolote". RC Mtanda.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema serikali ya Mkoa wa Mwanza imejipanga kikamilifu kudhibiti vitendo vyovyote vinayoashiria uharibifu au uvunjifu wa amani, Aidha amemuomba Katibu Mkuu huyo kufikisha salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa ndani ya Mkoa wa Mwanza amefanya makubwa sana.
"...lakini niseme tu kwamba fedha za miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mwanza katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake ni zaidi ya tirioni 4.2 zimetumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo" amesisitiza Mtanda.
"Mhe. Balozi Nchimbi kesho kwa kuwa una mkutano mkubwa nitapata fursa ya kuainisha miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo Rais wetu ameindeleza kwa mafanikio katika Mkoa wetu wa Mwanza. Ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa pia amemuhakikishia Katibu Mkuu huyo kuwa Chama cha Mapinduzi kuwa wanayo imani kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa hali ya usalama itakua kubwa na wananchi watashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo bila wasiwasi wowote ule.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.