RC MTANDA AWATAKA RUWASA KUTUMIA MBINU MBADALA UUNGANISHAJI MAJI UKEREWE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 27 Disemba, 2024 amekagua mradi wa Maji uliojengwa katika kijiji cha Bugula-Muriti kwa gharama za zaidi ya tshs. milioni 549 ambapo unalenga kuwanufaisha zaidi ya wananchi elfu saba katika vijiji vitano.
Akizungumza na wananchi baada ya ukaguzi huo Mhe. Mtanda amewataka Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kufanya tathmini ya kuongeza mtandao wa maji ili wananchi wa kijiji cha Ihebo ambacho ndipo kilipojengwa chanzo cha maji cha mradi huo yanapotoka waweze kuvuta maji hadi kwenye nyumba zao.
Aidha, ametoa wito kwa RUWASA kuona namna ya kuwaunganishia wananchi maji kwa kuchangia nusu gharama kisha malipo yanayobaki waendelee kulipa kwa kukatwa wakati watapokua wanalipia ankara za maji kwani kwa kufanya hivyo itaongeza msukumo wa wahitaji na hatimaye kutimiza lengo la Serikali.
"Wananchi wa kata hii ya Muriti msiwe na shaka maana Serikali inalenga kila mwananchi apate maji nyumbani kwake hivyo RUWASA wanakwenda kuweka utaratibu wa kuweza kuwafikia wote tena kwa gharama nafuu maana Serikali haifanyi biashara bali inatoa huduma." Mhe. Mtanda.
Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo Meneja wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Zubeda Said amesema utekelezaji wa mradi huo unahusisha tanki la lita 150, 000 vituo vya kuchotea maji pamoja na mtandao wa bomba wa Km 11.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.