Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Mhandisi Robert Gabriel amesema kuanzia Aprili 27 2022 Kikundi cha watu wachache Wamachinga waliovamia maeneo ya katikati ya Jiji warejee waliopangiwa tofauti na hapo Sheria itafuata mkondo wake.
Akizungumza na vyombo vya Habari Mkoani Mwanza,Mhandisi Gabriel amekitaka Kikundi hicho cha watu wakorofi wanaosambaza taarifa potofu na kurejea maeneo yaliyokatazwa waache mara moja na kutii Sheria bila Shuruti.
"Hali imeanza kuwa mbaya katika baadhi ya maeneo kutokana na baadhi ya Wamachinga kufanyabiashara maeneo yasiyo rasmi kiasi cha kuleta usumbufu kwa Wananchi" amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Amesema Kikundi hicho kinapotosha taarifa kuwa Mkoa umeliondoa Jeshi la Akiba siyo kweli bali walioondolewa ni wale wachache waliokiuka taratibu za majukumu yao.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamachinga nchini,Venatus Anatory amesema kitendo hicho wamekilaani kwani kisipochukuliwa hatua za Kisheria kitasababisha sura ya miji kuharibika
"Nimekuja Mwanza na kujiridhidha na maeneo rasmi waliyopangiwa Wamachinga,hivyo naunga mkono hatua za Kisheria kwa wale wanaokiuka taratibu hizo" amesema Kiongozi huyo wa Wamachinga.
Mkoa wa Mwanza upo mbioni kujenga Masoko ya kisasa ya Wafanyabiashara wakubwa, wakati na wale wadogo,mpango ambao utakamilika ndani ya miaka michache ijayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.