SUALA LA UPANDAJI MITI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA LIWE ENDELEVU:RC MTANDA
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mh:Christopher Ngubiagai ametaka kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake kwa kutambua umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea kuleta madhara makubwa duniani kwa sasa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru yaliyofanyika ki Mkoa wilayani Ilemela kwenye viwanja vya Halmashauri,comrade Ngubiagai amebainisha Dunia hivi sasa inashuhudia maafa makubwa ya mafuriko na kuangamiza maisha ya watu hii ni kutokana na athari za mazingira.
“..Uhuru ni haki ya msingi ya kila mtu au Taifa kuamua kufanya mambo bila kuingiliwa na mtu yoyote ki maamuzi,sisi watanzania hatuna budi kuendelea kuuenzi Uhuru wetu kwa vitendo likiwemo suala la utunzaji mazingira” Amesema Mkuu huyo wa wilaya akimnukuu hayati baba wa Taifa la Tanzania Mwl.Julius Kambarage Nyerere
Mhe:Ngubiagai ameongeza kuwa pamoja na shughuli mbalimbali ambazo zinafanyika katika maadhimisho hayo ni muhimu kuwaenzi waasisi wa Taifa kwa kuzingatia misingi ya uhuru ambayo inajumuisha umoja,usawa,uwajibikaji,kujitegemea na haki za binadamu ili kuleta maendeleo kwa kasi.
“..Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoendelea nayo ya kuleta maendeleo,kipindi cha uhuru mkoa wa Mwanza ulikuwa na shule 5 tu leo tuna jumla ya shule 332 na nyingine zinaendelea kujengwa."
Aidha Afisa usalama mstaafu wa mkoa wa Mwanza Dkt.Jacob Mutashi ametoa mada kuhusu amani wakati wa kongamano lililojikita zaidi katika masuala ya Uhuru wa Tanzania Bara, amesema nchi hiyo ilipata uhuru wake kwa njia ya amani bila kumwaga damu na kwamba nchi iliongozwa kwa kufuata misingi ya amani ,umoja na uadilifu bila kujali dini wala makabila ya mwananchi wake.
“.. Hatuna budi kuilinda tunu ya Taifa letu ambayo ni amani..” amesema Dkt.Mutashi
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mstaafu Dkt.Leonard Masale amesema Tanzania Bara inatimiza miaka 63 ya Jamhuri huku akifafanua maana jamhuri kuwa ni jamii huru
Maadhimisho hayo yaliyokwenda pamoja na kongamano la miaka 63 ya Uhuru na shughuli ya upandaji miti yamepambwa na kauli mbiu isemayo "Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.