Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Jenista Mhagama amewahakikishia wakazi wa Buchosa Wilayani Sengerema-Mwanza kuendelea kunufaika na miradi ya TASAF kwa kuletewa fedha Shs milioni 104.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Lushamba mara baada ya kufanya ukaguzi wa Kituo cha Afya,Waziri Mhagama amesema fedha hizo zimelengwa kwa wanufaika ilibwazidi kukuza shughuli zao za kujiongeza kipato kwa familia zao kwa kufanya ufugaji na shughuli nyinginezo.
Aidha, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa kukomesha tabia ya fedha hizo kutolewa kwa upendeleo na kuleta malalamiko kwa waliokusudiwa.
"Nimekagua kituo hiki cha Afya bado sijaridhika na Kasi yake, haiwezekani fedha zimeingia tangu Aprili mwaka jana hadi leo kituo hakijakamilika nataka ufikapo Machi 31 kiwe kimekamilika ili Wananchi wapate huduma".Amesisitiza Mhe. Mhagama.
Vilevile, ameahidi kuongeza majengo mawili ya Wodi ya wakina baba, mama na mtoto ili kituo kiweze kutoa huduma bora na kwa wananchi wengi..
"Mhe. Waziri tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu Dkt Samia kwa upendo huu tumepokea ruzuku ya Shs Bilioni 5.5 Wilayani Sengerema kwa ajili ya kunusuru kaya masikini na mipango mingine ya maendeleo, tutaendelea kumuunga mkono Mhe.Rais kwa juhudi hizo." Senyi Ngaga, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema.
Waziri Mhagama pia ametembelea Shule ya msingi Nyamimina ambako kuna mradi unaotekelezwa na TASAF wa ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili na Ofisi moja iliyogharimu Shs milioni 70.
Baada ya kupatiwa taarifa shule hiyo ina wanafunzi 1435, Waziri Mhagama ameongeza tena ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.