TUCHUKUE HATUA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MVUA NA UGONJWA WA KIPINDUPINDU: RAS BALANDYA
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka watalaam wa usimamizi wa Maafa na wadau kupanga Mikakati na kuchukua hatua kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu na athari za mvua za Elnino ilikuepusha majanga yanayoweza kujitokeza.
Akingumza leo Machi Mosi, 2024 kwa niaba yake Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Utawala na Rasilimali watu Daniel Machunda amesema bado inahitajika nguvu ya ziada kutoka kwenye mamlaka husika kudhibiti mifumo ya maji taka.
"Ugonjwa wa Kipindupindu ni rafiki wa uchafu, bado sehemu nyingi zinakabiliwa na changamoto hii tukiweka juhudi kwa kila taasisi husika tutautokomeza ugonjwa huu," amesisitiza Machunda.
Naye, Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa amesema makazi yasiyo na choo na sehemu zenye shughuli za wananchi na hakuna vyoo zinatakiwa zifanyiwe maboresho haraka iwezekanavyo.
“Tumewazuia mama lishe eneo la igombe kwa sababu walio wengi hawazingatii usafi kwenye kazi zao, na wakirudi wazingatie sheria za usafi” Mganga mkuu.
Kwa upande wake Afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa anayeshughulikia majanga Mhandisi Aaron Kalondwa ametumia kukwaa hilo kufafanua hatua za kuchukua kabla na baada ya majanga kutokea kwa wajumbe wa kikao kazi hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.