Leo Januari 20, 2024 Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa amekutana na makundi maalum kwa lengo la kuwapatia elimu na kuwataka kuchukua tahadhari zote dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu ikiwemo ulaji wa chakula cha mkusanyiko wa watu wengi.
Akizungumza nao kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa, amesema baadhi ya wagonjwa waliofuatiliwa walibainika kupata maambukizi hayo kutoka msibani hivyo ni vyema kuwa makini eneo hilo kwa kunawa maji yanayo tiririka na kuepuka kwa kipindi hiki kulala matanga.
"Ni lazima kila mmoja wetu atambue kilicho mbele yetu kwa sasa na tuzingatie usafi kwenye maeneo yanayo tuzunguka tukuzingatie yote haya visa vya mlipuko vitatoweka", amesisitiza Mganga Mkuu wa Mkoa.
Amesema tusiache jukumu hili kwa Serikali pekee bali kila mmoja awe makini na kutoa elimu hii kwa wengine ili jamii iendelee kubaki salama na kuendelea na majukumu ya ujenzi wa Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliyehitimisha mafunzo hayo mafupi ya utoaji elimu kwa makundi maalum amesema Kipindupindu kinapona endapo mgonjwa aliyebainika atafikishwa mapema kwenye vituo vya afya vilivyotengwa na matibabu yake ni Bure hivyo jamii yote izingatie miongozo yote ya tahadhari inayotolewa na wataalamu wa afya kwa lengo la kulinda nguvu kazi ya Taifa isipotee.
"Huu ni ugonjwa wa aibu yaani mtu kula kinyesi kibichi kinachotokea na vimelea,naamini mafunzo haya ya leo mliopatiwa yatakuja na matokeo chanya",Mkuu wa Wilaya Nyamagana.
Mratibu wa elimu ya afya kwa umna Mkoa wa Mwanza Leonald Mlyakado amebainisha Serikali inaendelea na zoezi la uelimishaji na kukagua maeneo yote yenye viashiria hatarishi na ugonjwa huo na kuchukua hatua za kitaalamu.
Mmoja wa wanufaika na elimu hiyo Alfred Kapore ameishukuru Serikali kwa utoaji wa mafunzo hayo kwani baadhi walikuwa hawana ufahamu wa kutosha kumtambua mgonjwa wa Kipindupindu na tahadhari nyingine.
Makundi hayo maalum yaliyonufaika na elimu hiyo ni walemavu,vijana,wanawake,wafanyabiashara wadogo na maafisa usafirishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.