TUNAHITAJI SULUHISHO KWA VITENDO NAMNA YA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA MALEZI : DKT. JINGU
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalumu Dkt. John Jingu leo mei 23 amefungua kongamano la malezi Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall, Mwanza na kuwataka wajumbe wa kongamano hilo kuja na mapendekezo ya majawabu halisia ya namna ya kuwa na malezi bora ya watoto.
Mhe. Dkt Jingu amesema anatamani kongamano hilo litakapokuwa likijadili lijikite katika kutafuta namna bora na wezeshi ya kuwalea watoto ambayo itawajengea msingi imara kuanzia ngazi ya familia, jamii na hata Taifa kiujumla.
“Wito wangu tuje na majawabu halisia, na siku hizi kuna smart phones, smart watches hivyo kwa nini na sisi tusiwe na smart child care?, kwa hiyo mapendekezo hayo ndio tunayoyataka”.
Awali akizungumza katika Kongamano hilo, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana ametoa rai kuwa jukwaa hilo lije na majibu chanya kwa familia kama nguzo imara katika kuwapa malezi bora watoto hapa nchini.
"Nitoe rai kwenu, kwanza mlitumie vizuri jukwaa hili vizuri kwa kuwa nyote mliopo hapa mnajihusisha na malezi kwa namna moja ama nyingine leteni mikakati chanya itakayokuwa na tija kwa Taifa” Amesema Katibu Tawala.
Kongamano hilo la malezi Tanzania lililobeba kaulimbiu isemayo “Kuwekeza katika maendeleo ya awali ya mtoto ni msingi wa kujenga Tanzania imara na endelevu” linatarajiwa kuhitimishwa hapo kesho tarehe 24 mei 2025 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.