UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA
Msemaji Mkuu wa Seiikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamadini, Sanaa na michezo Ndg, Greyson Msigwa amesema uzalishaji wa zao la Pamba mwaka huu 2024/25 umeongezeka kutoka tani 180,000 hadi 400,000 kutokana na jitihada za Serikali za mageuzi kwenye kilimo.
Akizungumza leo Mei 3, 2025 katika kipindi cha miaka minne katika kijiji cha Sayu mkoani Shinyanga, Msigwa amebainisha kuwa Rais Samia kwa kutambua umuhimu wa kilimo ameiongezea bajeti Wizara hiyo kutoka Tshs. Bilioni 200 hadi Trioni 1.
"Mhe Rais alisema bayana amedhamiria kuona kunakuwa na tija kubwa katika kilimo cha kisasa ili mkulima afaidike na kuongeza pato la Taifa kwa uhakika",Msemaji wa Serikali'
Msigwa ameendekea kubainisha ongezeko hilo la bajeti limeboresha maeneo mbalilbali ikiwemo ununuzi wa ndege Nyuki kwa ajili ya upuliziaji wa dawa ya kuuwa wadudu shambani.
Hali kadhalika, amesema Maafisa ugani wameendelea kujengewa uwezo pamoja na kupatiwa vitendea kazi vya uhakika ili waweze kuwafikia wakulima na kuwajengea uwezo wa mbinu bora za kilimo.
Msigwa akiwa mkoani Shinyanga ametelmbelea uwanja wa ndege uliipo eneo la Ibadakuli unaojengwa na kampuni ya Chikov kwa gharama ya zaidi ya Tshs. bilioni 44 na kutarajiwa kukamilka Juni mwaka huu.
"Serikali imejenga shule maalum za waichana 26 nchi nzima lengo kuwapata wataalamu wengi Wanawake hususan kwenye michepuo wa Sayansi", Amesema Msigwa akiwa katika shule ya wasichana iliyopo Old Shinyanga iliyojengwa kwa Tshs. billoni 4 .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.