VIJANA ZIDISHENI UBUNIFU ILI MKUZE KIPATO UFUGAJI WA SAMAKI KISASA: RC MTANDA
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mh. Christopher Ngubiagai amewataka vijana wanaojishughulisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kuzidisha ubunifu katika mradi huo ili kukuza mtaji na kuongeza kipato chao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na vijana hao mapema leo asubuhi Disemba 10,202 eneo la Kisoko kata ya Luchelele wakati wa zoezi la uvunaji wa samaki tani 2 kikundi cha Isingiti, Mh. Ngubiagai amebainisha uchumi wa bluu hivi sasa umekuwa mkombozi kwa vijana hivyo kazi iliyopo sasa ni kupanua wigo utakaosaidia kusonga mbele kimaendeleo.
"Serikali ya Rais Dkt.Samia imeweka mazingira mazuri katika sekta hii ya uvuvi,mikopo inayotolewa na benki ya TADB ni nafuu,hakuna tena sababu ya vijana kukaa vijiweni badala yake ni kuchangamkia fursa hii ili kujiletea maendeleo",Mkuu wa wilaya.
Aidha amevipongeza vikundi vya vijana hao kwa nidhamu ya urejeshaji wa mikopo kwa asilimia 100 hali inahofanya kuwepo kwa mzunguko mzuri kwa wakopaji wengine.
"Ndugu mgeni rasmi leo unashuhudia uvunaji huu wa samaki uliotokana na mkopo kutoka benki ya TADB wa zaidi ya shs milioni 122 uliotuwezesha kununua vizimba 8 kwa gharama ya zaidi ya shs milioni 33 na kupandikiza vifaranga 80,650 vilivyogharimu zaidi ya shs milioni 14,"Omari Mangu,Katibu wa kikundi.
Kwa upande wake Meneja wa benki ya TADB Kanda ya ziwa Samson Siyengo amesema jumla ya shs bilioni 4 zimetolewa kwa vikundi vya ufugaji wa samaki mkoani Mwanza na awamu ijayo watatoa shs bilioni 5.
Mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ulizinduliwa rasmi na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Januari 30,2024 kwenye uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.