Kitendo cha wafanyabiashara kupandisha bei vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na kirusi aina ya Corona ( COVID-19) kimewahathili baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Mwanza na kuachana na hali ya kujikinga kwa vifaa .
Hayo yalibainishwa na Nacy Kimaro mkazi wa Mbatini alipokuwa akizungumza na Gazeti hili alisema kitendo hicho kinachofanywa na wafanyabiashara ni kukomoana kwa sababu wanajua hali ya mtanzania ni duni hivyo walipaswa kuwa wazalendo baada ya kusikia ugonjwa umefika nchini wangeuza kwa bei nafuu kuliko ya awali.
Pia aliiomba serikali kuwapatia vifaa hivyo bure ambapo mtu akiitaji anaenda vituo vya afya na kupatiwa ili mwananchi ambao hawana uwezo wa kununua waweze kuvipata pia mbali na kuvipata elimu itolewa kila mara hasa maeneo ya sokoni ,stend , bar, ili kuwajengea uelewa na kuacha tabia ya kuupuza ugonjwa huu na kuuchukulia ni ugonjwa hatari na utaoweza kuleta maafa .
"Mbona Condom zinagawiwa bure na ukienda hospitali unazikuta zipo nje unaambiwa uchukue na wakati mwingine daktari anakupatia kabisa kwa nini hivi visipewe bure tena ukizingatia ugonjwa huu ni hatari kuliko magonjwa yote yaliyowahi kutokea na kuuwa watu wengi kwa wakati mmoja" alisema Kimaro.
Naye Kassim Omary mkazi wa Kangae mecco akizungumzia adha hiyo alisema kuingia kwa ugonjwa huo Tanzania imani na uhuru wa kutembea sehemu mbalimbali imepotea hivyo wamejawa na hofu pia kupanda kwa vifaa hivyo imegeuka kuwa changamoto.
Pia alisema,elimu itolewe juu ya matumizi sahihi ya vifaa hivyo na vinapaswa kuvaliwa kwa muda na wakati gani,maana imekua kila mtu anavaa tu kwa utaratibu wake.
" Sisi tunatembea bila kinga yoyote kwanza ukiangalia mimi nina familia ya watu 8 sasa maski moja ni 3000 ambapo kwa siku nitumie labda 28000 kipato changu ni elfu 2000 kwa siku hapo sitoweza bora selikali iingilie kati Rais kazuia mambo mengi yasifanyike kwa ajili ya ugonjwa huu sasa kwa nini hela hiyo isiingie kwenye kununua vifaa vya kujikinga na vigawiwe bure kwa wananchi " alisema Omary.
Naye Bahati Kazimili ni mumiliki na muuzaji wa duka la madawa Mecco alisema siyo kwamba wanapandisha bei kwa kupenda hiyo inatokana na sehemu wanapochukulia kwa bei ya jumla kupandisha bei hivyo kila mtu anaangalia kujiongea kipato .
" Siyo kwamba sisi atuguswi na hili janga lakini mazingira yanatufanya tuuze kwa bei hiyo mfano mwanzo tulikuwa tunatunua boksi moja la maski zikiwa 50 ndani kwa shilingi 15000 tulikuwa tunaziuza 1500 ambapo kwa sasa tunanunua boksi kwa elfu 80 hivyo inatulazimu kuziuza elfu 3000 kwa kila kimoja "alisema Kazimili.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dk. Thomas Rutachunzibwa alisema wamepokea taarifa ya watu kupandisha bei baadhi ya vifaa hasa wafanyabiashara wa vifaa vya tiba hivyo wamekuwa wakipita na kuwapa elimu ya kutokulichukilia suala hili kama fursa ya kupandisha vitu baadhi wameongea nao na wamewasikiliza.
Aliongeza kuwa kuna wafanyabiashara wengine wanatembeza vitakasa mikono (Hand Sanitizers) mitaani hivyo wamezikamata baadhi na kuzizuia zisitumike.
“Tuhimize wananchi kwamba hii ni vita lakini tunapokuwa tunatumia silaha lazima tuitumie kwa matumizi sahihi na siyo kuichukulia hii kama fursa na kuwaumiza wananchi hasa wale wanaohitaji kununua vifaa kwa bei nzuri lakini wanashindwa kutokana na bei kuwa juu “alisema Rutachunzibwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.