Mashirika yanayojihusisha na utoaji wa elimu kwa wajasiriamali Nchini na usajili wa bidhaa zao yametakiwa kwenda vijijini na kutoa elimu ili wajasiriamali wa pembezoni waweze kushiriki kwenye uzalishaji wenye ubora na kusaidia kukuza uchumi wa Nchi.
Amos Msakamali mshiriki wa mafunzo ya utoaji wa elimu kwa wajasiriamali yenye lengo la kuwasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitaweza kuuzwa ndani na nje ya nchi,wamesema kuwa baadhi ya wajasiriamali walioko pembezoni wanapopata mafunzo ya kuzalisha bidhaa hawafahamu kama kuna vyombo vingine vinavyopaswa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kabla ya kuingia sokoni.
“Elimu ndogo lakini tunatakiwa kwenda kuzalisha kwa viwango,leo mimi nimejifunza mengi, hii itanisaidia kwenda kuzalisha kwa ubora zaidi,ushauri kwa Serikali wawafikie watu ambao wapo nje ya miji maana kule nako kuna wajasiliamali wengi ila hawapati elimu hii”,alisema Amos. .
Naye Nuru Mwasulama ambaye ni Mkaguzi wa chakula na dawa kutoka TFDA amesema kuwa TFDA inashiriki kikamilifu katika kuwajenga wajasiriamali na kuhakikisha kuwa uzalishaji wa bidhaa zao unakuwa salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
“Kwetu sisi TFDA usalama wa bidhaa ni kitu cha kwanza ambacho tunasema hakiwezi kufumbiwa macho wakati tunaendelea kuwahudumia wajasiliamali tunahakikisha watanzania wanapata bidhaa salama kwa kuwa rasilimali ya Nchi ni watu hivyo lazima wawe salama”,alisema Nuru.
Nickonia Mwambene ni Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS amesema kuwa Serikali imewarahisishia wajasiriamali kupata huduma mbalimbali ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kuzalisha bidhaa zao na kukuza uchumi wa Nchi.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wajasiriamali wapatao 100 kutoka katika Mkoa wa Mwanza na imetolewa na TBS kwa kushirikiana na mamlaka ya chakula na dawa (TFDA), Shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO) na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.