Washauri wa baraza ardhi na nyumba wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ,kuepuka vishawishi vya rushwa ,kufuata kanuni taratibu na sheria za ardhi ili kujenga imani kwa jamii.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya kuapisha washauri wa baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Sengerema alisema idadi ya migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi imeendelea kuongezeka siku hadi siku.
Hivyo baraza hilo litapokea na kutatua migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mbayo inatatuliwa kwa uharaka na kuhakikisha haki inapatikana ili kuchochea maendeleo kwa wananchi.
Amesema awali wananchi walikuwa wakienda kupata huduma katika baraza la Geita ,kwa sasa watapata kwa urahisi hivyo viongozi waepukane na vishawishi vya rushwa watumie uzalendo na kuwa sababu ya faraja na utatuzi na kutokuwa chanzo cha migogoro.
" Mkoa unajukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora inayotolewa kwa ueledi na uadilifu hivyo utatuzi wa migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi mhakikishe mashauri yanasikiliza na kuisha katika kipindi kisichozidi miaka miwili tangu shauri kufunguliwa katika baraza" alieleza Mkuu wa Mkoa.
Pia amezitaka alimashauri zote mkoani humo kuhuisha mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji kwa yale yaliyomaliza muda wake kutoa elimu kwa wajumbe wa mabaraza hayo ili kuboresha utoaji wa huduma pia wananchi watumie huduma hizo kikamilifu kupata ufumbuzi wa migogoro yao kwa mujibu washeria.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Senyi Ngaga alisema kati ya wananchi 100 anaowasikiliza asilimia 85 hadi 90 wote wanalalamikia migogoro ya ardhi hivyo baraza hilo litageuka chachu ya kupunguza migogoro hiyo pia kuwapumguzia wananchi umbali mrefu wa kufuata huduma hiyo mkoani Geita.
Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis Tabasamu amesema kipindi cha Mhe. kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana alikutana na malalamiko ya wananchi kutembea umbali mrefu kutafuta haki kwenye baraza la ardhi Wilaya ya Geita,kuwapo kero hiyo na malalamiko mengi aliamua kutafuta ofisi ya kwa ajili ya baraza hilo kufanyia kazi zao.
"Kwa kushirikiana na Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema tukaamua ofisi ya mtendaji wa tuifanyie marekebisho ili itumike kama ofisi ya Baraza la Ardhi la Wilaya ya Sengerema, Jumatatu ya wiki ijayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza atakuja kulifungua,'' alisema
Akiwaapisha wajumbe hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel alizitaka halmashauri zote mkoani humo kuhuisha mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.