NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kiwango cha ulaji wa samaki kwa watanzania bado kipo chini sana licha ya taifa kuwa na maziwa, mito, bahari na mabwawa ya wafugaji.
Amesema takwimu zinaonyesha ulaji wa samaki kwa mtanzania ni kilo nane kwa mwaka ukilinganisha mapendekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba inapaswa kuwa kilo 20.
Kauli hiyo aliitoa jana jijini Mwanza wakati uzinduzi wa kadi ya Uvuvi jijini Mwanza uliofanywa kati ya Benki ya Posta Tanzania (TPB) na Chama Kikuu cha Ushirika wa Wavuvi Tanzania (Chakuwata) baada ya kuingia makubaliano ya kukopeshwa pesa ikiwa lengo ni kurasimisha kundi hilo na kuwakwamua kiuchumi.
Ulega alisema anashangazwa kuona kiwango cha ulaji wa samaki kikiwa chini sana licha ya Tanzania kuwa na maziwa,mito, habari na mabwawa ya ufugaji ambapo aliongeza kuwa takwimu zinaonyesha samaki waliovuliwa mwaka jana ni tani 450,000 huku mahitaji ni tani zaidi ya tani 700,000.
“Tangu hafla hii ianze hapa sijaona wavuvi mnacheka au mnafurahi maneno yanayozungumza na viongozi, najua hamu yenu ni kutaka kusikiliza kama Serikali itakuja na tamko mbadala wa kuruhusu mtumie zile nyavu tulizozikataa, pia natambua mnatumia sababu ya kwamba nchi zile za uoande wa pili zinaendelea kutumia nyavu ambazo sisi Tanzania tumezizuia.
“Sheria za makubaliano tulipitisha nchi zote, sasa kama upande wa pili bado hawazingatii sasa tamko letu kama Tanzania sisi tunaendelea kusimamia sheria lakini haitoshi bado tunafuatilia kwa ukaribu kuona kinachofanyika huko upande wa pili, vile vile mkitaka nitangaze leo nyavu zile zitumike itakuwa ngumu kwangu maana zipo taratibu za kubadilidha sheria, hivyo kuweni na imani jambi hilo litakaa sawa.
“Leo tumekutanishwa hapa kwa jambo kubwa sana ambalo tumeona nyinyi wavuvi mnapaswa kuwezeshwa ili kufanya shughuli hii kwa kutumia vifaa vyenye ubora, hivyo Benki ya TPB imekuja hapa kwa ajili ya kuwatambua mtu mmoja mmoja na kikundi, ndio maana mnaingia makubaliano kupitia chama chenu, tunataka kiwango cha ulaji wa sakimi kitoke kilo nane kwa mwaka kifike angalau kilo 20 zinazopendekezwa na WHO,”alisema.
Ulega alisema bado haamini takwimu zinazotolewa kwamba sekta ya uvuvi inachangia pato la taifa kwa asilmia 1.7 ikiwa inashina nagasi ya nne ambapo aliwataka wahusika wa kukusanya takwimu kufanya unyambulisho wa matumizi ya samaki kuanzia minofu yake, mifupa, utumbo, mabondo, matamvua na vitu vingine.
Alisema kitendo cha Benki ya TPB kuingia makubaliano na Chakuwata na kuwakopesha mvuvi mmoja mmoja na kikundi kitawezesha samaki wa kiwango kivuliwa kwa kuwa kutakuwa na vifaa nyenye ubora huku akiweka imani ya kiwango kuongezeka cha ulaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema ikiwa taasisi za fedha zitasogezwa kwa wananchi, itakuwa ni rahisi taifa kupambana na umasikini na kufanikiwa kukwamua jamii kwa pamoja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.