Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongella, amewaonya na kuwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi pamoja na kutatua kero za wananchi.
Mhe Mongolla aliitoa onyo hilo katika kikao cha upokeaji taarifa ya utekelezaji wa zoezi la uanzishwaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi Tanzania (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoa wa Mwanza.W
Mhe Mongella alisema, Kila mtumishi akifanya kazi bila visingizio, kuwajibika kwa nafasi yake na kutekeleza mipango na maelezo ya Serikali, suala la wananchi kujitokeza na mabango ya malalamiko kwa viongozi wa Kitaifa litapungua.
“Sipendezwi na mabango ya wananchi yanayoonesha awatatuliwi kero zao, na yeyote atakayezembea kuwahudumia wananchi kwa nafasi yake na malalamiko yakajitokeza kwa viongozi wa Kitaifa atawajibishwa”,alisema Mhe Mongelle
Aliongeza pia, wapo baadhi ya watumishi wanakwamisha mipango ya Serikali kutokana na tabia yao ya kuwa na visingizio vingi, kutaka wabembelezwe kutimiza wajibu wao na kuwataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mkoa wa Mwanza kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi kila baada ya miezi mitatu.
“Twendeni vijijini tukawahudumie wananchi, mfano katika hili la saratani linakwamisha sana maendeleo kwani mama mmoja akiwa na saratani lazima familia itayumba hata kama wana uwezo wa fedha, tambueni asilimia 80 ya shughuli za nyumbani zinafanywa na mama,bila kusimamia afya na uhai wa watu tutakuwa tunajidanganya kupata maendeleo”alisema
Naye Afisa wa Mpango wa Taifa, Kitengo cha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi Tanzania (HPV) kutoka wizara ya afya, Pricilla Kinyunyi alisema kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha jumla ya watanzania 50,000 wanapata maambukizi mapya na asilimia 70 ya wagonjwa hao wanajitambua wakiwa katika hatua ya nne ambayo ni hatari.
Alisema asilimia 36 ya wagonjwa hao waliogundulika na saratani wanapoteza maisha, hivyo aliwashauri wazazi kuwatunza mabinti wao na kuwashauri kuepuka kuanza ngono mapema sambamba na kuwahimiza kupata chanjo wanapofikisha umri wa miaka 14.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.