Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Jenista Mhagama ametoa rai kwa watumishi wa Umma wilayani Magu kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi ili kuboresha huduma za kijamii.
Amesema Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipambanua kuwahudumia wananchi kwa
viwango vya ubora wa juu hivyo ni wajibu wa kila mtumishi wa umma kujituma katika kusimamia miradi na kuhudumia wananchi ili wananchi wapate huduma bora za kijamii kama Maji, Afya, Elimu na pembejeo za Kilimo.
"Wananchi wakisema wanapata huduma nzuri basi ni mazao ya utumishi bora wa umma na wakilalamika basi ni zao la kutowatumikia vizuri, nawaomba tuwe na utumishi wa umma unaojali haki na wajibu kama Rais Samia mwenyewe alivyoagiza wakati akilihutubia Bunge kwa mara ya kwanza." amesema Waziri Mhagama.
Ndani ya miaka miwili watumishi 116792 wamekwishalipwa madai ya mishahara, nakuagiza Mkurugenzi kupitia maafisa Utumishi wako kuendelea kulipa madeni ya watumishi kupitia mfumo wa digitali ambao una ufanisi mkubwa hususani watendaji wa vijiji na kata ambao waliondolewa kazini na kurejeshwa mwaka 2017/18.
"Kwa miaka karibia saba, watumishi wa Umma tulikua hatujapandishiwa mshahara lakini ameingia mama ametuongezea kwa asilimia 23 hivyo tunamshukuru sana Rais Samia kwa upendo huo na ametuboreshea sana mazingira ya kazi kwa sasa", Amesema Daniel Sanyenge, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) wilaya ya Magu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.