WAZIRI MKUU ATUMIA JUKWAA LA MAADHIMISHO YA MUUNGANO KUKAGUA MIRADI UKEREWE
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Aprili 25, 2025 amefanya ziara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kwa kufanya ukaguzi na kuweka jiwe la msingi katika miradi miwili inayotekelezwa na Serikali ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya muungano ambayo kilele chake ni Aprili 26 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa mkutano maalum na wananchi kwenye uwanja wa Getrude Mongela mjini Nansio, Waziri mkuu amesema mwaka huu hakuna maadhimisho rasmi ya sherehe za muungano na badala yake viongozi wanafanya shughuli za kukagua miradi ya maendeleo kwa wananchi kama anavyofanya hapa Ukerewe.
Awali kabla ya mkutano huo maalum, Mhe. Waziri Mkuu amefanya ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa iliyopo kijiji cha Bulamba kata ya Bukindo kwa gharama ya T shs bilioni 25,Waziri mkuu amewapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kutoa hekari 16 bila fidia ili kupisha mradi huo mkubwa
"Nyie kweli ni wapenda maendeleo,Serikali inapata changamoto sana inapotaka kufanya miradi ya maendeleo wananchi kushinikiza malipo ili kupisha maeneo yao huku wakitoa sababu mbalimbali",Waziri mkuu.
Akiwa njiani kuelekea mkutano maalum,ameweka jiwe la msingi na kufanya ulaguzi kwenye jengo la Halmashauri ya Ukerewe linalojengwam kwa gharama ya zaidi ya T shs bilioni 3.
Aidha Waziri mkuu akiwa kwenye mkutano maalum wa hadhara ametumia jukwaa hilo kuwakumbusha wananchi kuendelea kuuenzi muungano ulioadisiwa na Hayati Mwl Nyerere na Abeid Karume huku Serikali zote zikiendelea kuwapigania maendeleo wananchi wake.
"Ndugu wananchi katika mkutano huu wa kuelekea maadhimisho ya muungano nipo na wataalamu mbalimbali ambao watafanua hoja ambazo ni changamoto 'katika miradi yenu ya maendeleo,naanza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tamisemi,Mhe.Festo Ndugange anayesimamia afya,"Mhe.Majaliwa.
Katika salamu zake za Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Mkoa huo,Mhe.Said Mtanda ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuleta miradi mingi mkoani humo na hasa wilayani Ukerewe.
"Mhe.Waziri Mkuu kutokana na jiografia ya wilaya hii wananchi wamekuwa wakipata tabu kuja kupata matibabi mjini Mwanza au hapa Nansio,lakini sasa kukamilika kwa hopitali ya rufaa itakuwa ni mkombozi kwao,"Mtanda
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.